Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Gazeti la Mwananchi limeripoti muda mfupi uliopita kuwa Msemaji wa Klabu Simba Haji Manara alizimia mara kufuatia kipigo cha bao 4 kwa bila kutoka kwa Klabu ya Kaizer Chief ya Africa Kusini
Inaarifiwa kuwa Msemaji huyo maarufu wa Wekundu wa Msimbazi hakuamini kuwa timu yake inaweza kufungwa kwa magoli mengi hivyo ukizingatia uimara na ubora wa kikosi cha Simba
===
ILIKUWA siku ngumu kwa Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Sunday Manara baada ya kuzimia mara mbili katika hoteli ya Sky ambayo Simba ilikuwa imefikia jijini Johannesburg kufuatia kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Kaizer Chiefs.
Manara alianza kujisikia vibaya mara baada ya kuwasili hotelini akitokea katika
Uwanja wa FNB ambako pambano hilo lilifanyika. Madaktari wa Simba walilazimika
kumpa huduma ya kwanza kwa saa zima msemaji huyo ambaye ni mtoto wa staa wa zamani wa Yanga, Sunday Manara
“Nimezimia mara mbili. Hali yangu ilikuwa mbaya nusura nife. Nina presha ya kushuka na mara nyingi huwa natumia chumvi kujiweka sawa. Hali yangu kwa sasa ni nzuri lakini huu mpira unaweza kutuua siku moja,” alisema Manara.
Simba ilikubali kichapo hicho na kujiweka katika mazingira magumu ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika huku pambano la marudiano likitazamiwa kufanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Advertisement