Haji Manara: Bunge liingilie kati sakata la mechi baina ya Simba na Yanga

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Ameandika hHaji Manara



Kabla ya jambo lolote lile kuendelea iundwe Kamati ya kibunge ijiridhishe kuhusu jambo liliotokea leo,ambalo limeacha maumivu makubwa Kwa Washabiki wa soka nchini zaidi ya elfu arobaini ambao walishalipa viingilio vyao ili kuangalia mechi hyo, lakini pia liliochafua taswira ya nchi kimataifa ukizingatia nchi nyingi za Afrika zilikuwa zimejiandaa kuangalia game hii!!
Baadhi ya hadidu rejea za tume hyo huru ziwe hz!!

Nn kilisababisha mechi hii kusogezwa mbele Kwa masaa mawili?

Why game Yanga na Azam pamoja Yanga na Biashara Mara ambazo nazo zilisogezwa mbele masaa mawili zilichezwa ila hii ya leo imeshindikana kuchezwa?

Uwazi wa kile kilichosababisha mechi isogezwe mbele Kwa masaa mawili na kwa nn Yanga muda mchache baada ya taarifa hyo kutolewa walitoa taarifa ya kuonyesha kutaka kugomea hyo mechi?
Je kwa nn ugomeaji huu uwe leo na usiwe ktk mechi za Azam au Biashara?

Na kama Serikali ilikuwa na sababu za msingi za kusogeza mbele muda wa mechi Kisha kuiarifu TFF (@tanfootball) na Shirikisho hilo kuviandikia vilabu vyote barua,,Kwa nn Yanga pekee wagomee? Na kama wamegomea why Simba haikupewa ushindi?

Je hakukuwa na mbinu ya makusudi ya kuhairisha hii mechi?
Kama ilikuwepo nn kitaendelea?

Nani atalipa gharama ambazo klabu zimeingia kujiandaa na mechi hii na nani atalipia gharama za Watanzania waliolipa viingilio vyao sambamba na gharama kwa wale waliotoka nje ya Dar?

Hil jambo lisichukuliwe kirahisi rahisi maana limeacha maswali mengi ambayo Watanzania waliolipa viingilio vyao na wale walionunua vifurushi vya azamtvtz wanapaswa kujua, lakini pia limeitia doa ligi yetu ambayo kwenye siku za Karibuni imekuwa maarufu kote barani Afrika.

@bunge.tanzania la watu linao wajibu wa kusimamia kero za watu kama hz za leo,,,ni wao pekee kwa sasa wanaweza kuja na majawabu sahihi juu ya kadhia hii iliyowaumiza Watanzania wengi.

@bunge.tanzania
 
Kwani wao TFF wanasemaje sio uyu msemaji wangu wa Simba bora atulie tu na kusubiri.
 
Pumbafu sana TFF.
Kwa nini mnawalinda watu kwa kuitaja TFF? Kuweni wazi, pelekeni shutuma zote kwa Wizara. Haya mambo ya kufichiana aibu ndio yatawapa kiburi maana watajua wabongo ni rahisi zaidi kuikabili TFF kuliko muhusika
 
Hizi timu mbili (simba na yanga)+ uongozi mbovu wa soka+ siasa kwenye soka = kufeli kwa maendeleo ya soka Tanzania
 
Kwahiyo bunge ndio linaamua kila kitu?
 
Ndio athari za kuruhusu upumbavu wa Ndugai, we said it Ndugai akiachiwa aisigine Katiba kuna wapuuzi wengine watakuja kufanya upuuzi mwingine. Na huu ni mwanzo tu, kama kila mtu anamuogopa kumkemea Ndugai tutarajie makubwa
 
Manara angekaa kimya kuliko kutoa hayo maboko kwa sheria gani bunge lina ingia kwenye mambo ya mpira?
 
Yaani Manara hajistukii kuwa hizo mechi zote anazozitolea mifano zilikuwa za Yanga?
Hajiulizi kwanini ni mechi za Yanga tu ndizo husogezwa mbele!?
Hajiulizi kuwa huenda Yanga wamechoshwa na huu upuuzi na leo wameamua kung'ata panapouma!?

Manara sijui anakwama wapi kushindwa kuelewa kile anachokiandika mwenyewe.
 
Mimi ni simba huyu manara kaandika upumbavu nae ni bwege kama bwege wengine
 
Huyu Manara hana anachojuwa, yeye Ni kuropoka tu kila linalokuja mdomoni mwake bila kushirikisha ubongo.
 
Manara makelele ila mpira haujui,ila si shangai hata Mexime aliliongea huu mpira wetu unaongoza na vilaza.Sasa haoni jambo hili ndio analikuza,kwani hili jambo likifika FIFA TFF na Tanzania zinapigwa pini hazito shiriki michuono yote.

Yanga wapo sahihi ktk hili.
 
Bunge halitakiwi kuingilia hii issue kwasababu maamuzi yatayotoka huko yanaweza kuwa ya kinazi.
 
Hivi kuna mtu yeyote ambaye amemwelewa Manara maana naona kama ameandika katikati ya mstari (hayaeleweki)!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…