Haji Manara hana mipaka katika kazi yake

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari zenu wakuu,

Poleni na majukumu na mihangaiko ya kila siku ya kutafuta riziki hasa kipindi hiki cha nchi yetu kuingia uchumi wa kati.

Kwanza nianze kwa kuweka wazi kabisa mimi ni shabiki wa SIMBA SC ila baadhi ya mambo ambayo yanafanywa na manara ni udhalilishaji na ya kipuuzi kabisa

Baadhi ya posts zake kwenye mitandao ya kijamii ni za kejeli vijembe na dharau kwa watu na team pinzani, baada ya mchezo Kati ya Simba Queen's na yanga aliweka Post ya mwanadada mchezaji wa yanga akiwa chini akiambatanisha na kijembe na picha yake akiwa ameweka emoji kwa nyuma ambayo kwa kawaida ukiangalia hakukuwa na haja ya kufanya vile zaidi ya kutoa matokeo tu ingetosha.

Baada ya mchezo wa juzi Kati ya Simba na yanga mchezo ambao Simba aliibuka na ushindi wa bao 4-1 yanayoendelea kwenye kurasa zake za kijamii na anayoendelea kuyaongea ni kejeli mipasho na dharau kwa team pinzani kitu ambacho hakina ulazima wa yeye kufanya hayo yote.

Hivi ukiwa msemaji wa team ndo unatakiwa ufanye kama mambo anayofanya manara ili uwafurahishe watu hamna njia nyingine cha ajabu kila mtu anafurahia anacho fanya hakuna hata wa kumshauri akiwemo na MO mwenyewe ana support anayofanya manara kwa team pinzani na baadhi ya watu wengine.

Kilichonifanya niandike huu Uzi kuna video amepost manara kwenye page yake ya Instagram ikimuonyesha shabiki wa yanga akiwa anatokwa na haja ndogo wakati wa mechi ya Simba na yanga ya juzi kwa umri na kwa nafasi yake Kuna vitu anakosea Sana kwa influence ambayo anayo kwenye jamii hana mipaka katika Kazi yake.

N.B……… simpangii Cha kupost wala jinsi ya kuishi ni mtazamo tu
 
Mkuu pamoja na yote hayo umeongopa kwenye kitu kimoja wewe sio Shabiki wa Simba ni Shabiki wa Yanga.

Pole sana hata sisi mlivyotufunga tuliumia hivyo hivyo.
Yaaan wee acha tyuuuh dea.
 
Kaa kwa kutulia, hakuna namna, muache manara afanye anavojisikia.
 
Mie ni shabiki wa Yanga ila nafurahi na inaleta hamasa nkiona post za Haji Manara na naamini ni funzo tosha kua tujenge timu yetu uzuri ili tulete upinzani kwa simba. Sijaona chochote kibaya zaidi ya kututia hasira sisi wana yanga tufanye usajili mzuri ili tusipitie tena dhahama kama hii. Ata sisi tulipowafunga ilikua ni sherehe kwa kila mwana yanga na tuliwakera sana wana simba.
 
Mkuu Ila manara kazidi
 
Alivyoitwa mwalimu wa madrasa aliwaita waislamu wote duniani wamsaidie..kwanza ni mlemavu alafu anawatoa kasoro watu...kama yule dada wa Yanga alimdhalilisha sana
 
Alivyoitwa mwalimu wa madrasa aliwaita waislamu wote duniani wamsaidie..kwanza ni mlemavu alafu anawatoa kasoro watu...kama yule dada wa Yanga alimdhalilisha sana
Akitaniwa huko anaomba huruma kila media
 
Mimi sioni kama kuna shida sababu anapost kwenye account yake binafsi na wala sio account ya club
 
Mkuu hilo ni funzo kama wewe una moyo wa kike usiangalie dabi , kama jamaa katokwa mikojo nasubiri siku mtu atakapo tokwa na uharo, nakukumbusha kwa kuwa ni account yake baasi hana mipaka labda avunje sheria za jamhuri
 
hivi ukimtania haji kulingana na hali aliyonayo ya ki-gene inaweza leta shida?
 
Huyo atawapa watu dhambi za bure maana hachelewi kusema anabaguliwa kisa ni mlemavu wa ngozi.
 
Mkuu pamoja na yote hayo umeongopa kwenye kitu kimoja wewe sio Shabiki wa Simba ni Shabiki wa Yanga.

Pole sana hata sisi mlivyotufunga tuliumia hivyo hivyo.
Yani wewe ndio umemaliza kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…