Haji Manara(HM) na Mechi ya Karne Yanga na Simba Nyamagana 1974

Haji Manara(HM) na Mechi ya Karne Yanga na Simba Nyamagana 1974

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Msikilize HM akikurudisha nyuma zaidi ya miaka 40 akieleza "Mechi ya Karne" kwa Tanzania pale Young Africans walipokutana na Simba kwenye Fainali ya Club Bingwa Uwanja wa Nyamagana, Mwanza mwaka wa 1974.

HM anakuchukua katika safari ndefu ya maandalizi ya mechi hii kutoka Dar es Salaam kukufikisha Afrika ya Magharibi, Ulaya na Amerika ya Kusini.

HM anaeleza kuwa Yanga na Simba hazikuwa club za maskhara.

Msikilize HM anavyokunyambulia nguvu kubwa za kiuchumi walizokuwanazo club mbili hizi zilizoweza kujenga timu kali zilizotetemesha club maarufu za Afrika zikitangaza jina la Tanzania kote walipofika kucheza mpira.

HM kwa ufundi wake wa kuchora picha ndani ya mazungumzo yake anaeleza nafasi ya "Saikolojia," na "Wababe," katika mpira na nafasi ya "Wazee wa Club."

Huwezi kusinzia HM anapozungumza na wewe.

Karibu...

 
Back
Top Bottom