Haji Manara: Mo alitaka niwe balozi wa bidhaa zake badala ya Azam. Asema Mo anadai hapati faida ilhali jezi za Simba zimejaa matangazo yake

Tumuache aruke ruke haina haja ya kumjibu
 
Umeijenga brand ya simba_ Yes ahsante kwa hili, ila umesahau kuwa simba ndio imekujenga wewe zaidi kuliko ulivyoijenga.
Hujawahi pewa bonus wanapewa wachezaji tu_ Vipi, kuna viongozi wanapewa bonus, kama viongozi wanapewa bonus basi ulistahili.....
[emoji1533][emoji1533][emoji1533][emoji1752][emoji1752][emoji1752]
 
Well said brother. Manara ni mtu hovyo kuwahi kutokea. Sema ujinga wa watanzania wachache ndiyo silaha yake. Yaani msemaji anataka yy ndio awe front line haaaahhhh ya nchi gani hiyo..? Uswahili mwingi. Miko na maadili ya kazi izingatiwe. Manara kajengwa na simba ndio maana linaumia maana kile alichotegemea kitashindwa hivi hajui tuliishabikia simba hata ilikua simjui.
 
Simba ipo miaka na miaka kajenga brand ipi huyo manara, yeye ndo kajijenga kwa kutumia Simba.
 
Manara anajivunia mikataba nje ya Simba.
Bila kutambua kuwa Simba ndio imempa umaarufu hadi ikampaisha kuhitajika kutumika na kampuni nyingine.
Mbona kabla ya kuwa Msemaji wa Simba hakuna kampuni zilizompa mikataba.
Tatizo la Manara ni Kujikweza.
Cheo cha Usemaji, ni cheo cha kawaida sana.
Manara anataka awe juu ya viongozi wote hapo Simba.
Amzidi hadi Mtendaji Mkuu, hadi Muwekezaji mwenyewe.
Manara hata anapoongea ana Kibri kikubwa.
Ona alivyomfokea yule Mwandishi wa habari bila sababu.
Kufanya kazi na mtu kama Manara anayependa kujikweza ni ngumu sana.
Anasema hakuwa na mkataba hapo Simba, hivi kazi ya Usemaji inafanywa bila mkataba ?

Kama anafikia kumsema kwa dharau Bilionea MO, mtu ambaye alikuwa naye karibu sana, kiasi cha kuweza kuomba nafasi ya kukutana naye na kumweleza shida zake kwa upole na kusikilizwa na hakufanya unategemea atamheshimu nani ?
Sasa hivi inasadikiwa anawaheshimu Bakhresa na GSM tu.
 
Hapo zingatia neno MIKATABA ...! Hii ina mwisho wake na aliyekupa mkataba ukikoma ana hiari ya kukuongezea ama LA...Je baada ya hapo nini kitafuata ITV? Tuuache muda utasema
 
Manara na chama

Hii bond si bure
Siyo Chama tu wachezaji Karibu wote.Ukigombana na Manara ujue umegombana na wachezaji wengi na baadhi ya wajumbe wa benchi la Ufundi .Muda utasema tujiandae kisaikolojia
 
Mgogoro wa Simba na Mohamed Dewji kuna mkono wa nje ya Mpira

Haji Manara kwa mujibu wa maelezo yake kavumilia mengi sana ikiwemo kufanya kazi miaka 6 bila ya mkataba, kujisafirisha kwa gharama zake kwny safari za kikazi na mambo kadhaa wa kadhaa, ilikuaje akashindwa kuzuia hasira zake kwa jambo dogo tu la kuambiwa uneonekana kwa Gharib wakati si dhambi na mara kadhaa amekuwa na gharib?

Mkono mkuu unamtumia Haji kuhakikisha Simba inarudishwa kwa Walalahoi
 
Kwani kuwa Mzaramo ni kosa?
 
Reaping where you have not sown is Challenging. Rest in Peace Hajji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…