OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Jana huyu mpayukaji aliitia press conference isiyo na kichwa wala miguu. Press conference isiyo na ajenda yeyote zaidi ya kupayuka na kupovuka.
Kama kawaida yake,katika kutoa povu amejikuta anaijadili Simba Sc. Kwamba hata yeye anatamani Simba Sc ishinde kombe la CAF.
Hatutaki maombi ya kinafiki. Juzi tu uliandika kwenye mitandao ukiuambia umma kwamba ushindi wa Simba Sc hutegemea mbinu chafu na ukawaelekeza wapinzani nini cha kufanya. Hayo mapenzi na Simba umeyatoa wapi? Umewahi kuomba radhi kwa hilo?
Ameenda mbali zaidi na kumbeza Ahmed Ally kuambatana na mashabiki katika kuhamasisha mashabiki kwenda uwanjani. Anasema hawezi kupanda lori. Upande lori kwenye jua kwa afya gani uliyonayo? Ukipiga route moja tu kwenye jua kali tunakuzika
Huyu mtu ana mizigo mingi sana ameibeba, mizigo ya kufitinisha watu, mizigo na uzushi na umaarufu wa kukashfu. Mizigo ya ndoa na umaarufu kunuka.
Namshauri ahangaike kuitua mizigo aliyobeba badala ya kuhangaika na Simba Sc