Haki elimu nao watoa kauli sakata la kufutwa matokeo ya kidato cha nne

Haki elimu nao watoa kauli sakata la kufutwa matokeo ya kidato cha nne

babumapunda

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
4,643
Reaction score
3,301
HakiElimu YAKATAA KUFUTA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE.

SERIKALI imetakiwa kuacha kukurupuka kufuta matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 kutokana na sababu za msingi za kufeli kwa wanafunzi hao zinafahamika.Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na muungano wa asasi tano za kiraia uliowakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu,Elizabeth Missokia.

Asasi zilizotoa tamko la pamoja huku zikipendekeza njia sahihi ya serikali kuwekeza katika elimu ni pamoja na Hakielimu yenyewe, Policy forum, Sikika, TenMet na TGNP.

Kwa niaba ya mitandao hiyo mkurugenzi huyo alisema hakukuwa na haja ya kufuta matokeo hayo na kufanya maboresho kwa kuwa
sababu zilizosababisha kufeli kwa wanafunzi zinajulikana na si kama serikali inavyodai kwa sasa.

Missokia alisema kabla ya serikali kutoa uamuzi huo ilitakiwa kuweka wazi mapendekezo ya Tume ya Waziri Mkuu iliyoundwa kuchunguza matokeo hayo ili wadau wa elimu wapate fursa ya kuona sababu zilizochangia kushuka kwa ufaulu katika mitihani hiyo.
 
Hii ndo tz bhana. Ni upepo tu utapita.
Wala wasijisumbue maana serikali hii sikivu imeziba masikio na macho. Ole wao watz
 
Hii ndo tz bhana. Ni upepo tu utapita.
Wala wasijisumbue maana serikali hii sikivu imeziba masikio na macho. Ole wao watz
 
Serikali inafanya ujinga mkubwa sana maana umeona kama vile balaza la mtihani limefanya makosa kutoa matokeo hayo. Naiomba serikali ijaribu kuangalia pande zote mbili maana haiwezekani wanafunzi waliofeli wakalazimisha wafaulu, hiyo tuhesabu kwamba imepita ila tuangalie mbele na tutafute njia zitakazo wezesha wanafunz wawe wanafanya vizuri ili tupate wataaram wa mambo mbalimbali hapo badae na si kuzalisha MAMBULULA.
 
et watarudisha nyuma grade za ufaulu!!!! Hii ni sawa na kupanua goli uwanjani kila mchezaji afunge(hata golikipa).
 
Back
Top Bottom