Haki ya mpangishaji iko wapi? Naombeni msaada wa kisheria

Yohana Daniel

Member
Joined
Mar 18, 2018
Posts
63
Reaction score
33
Habarini za uzima ndugu zangu

Husika na kichwa cha habari hapo juu, naomba Niende moja kwa moja kwenye mada nilikua na mpangaji ambae alilipa pesa ya kodi yake vizuri wakati anaingia shida ni pale tu ilipoisha hakuweza Kulipa tena nikampa notice ya kuhama free bila kunilipa chochote ila huu ni mwezi wa tatu tangu amefunga kufuli lake kwenye chumba changu

Sasa naomba kufahamu najua anaweza kuwa ametega tukibomoa tu atataka kulipwa maana anaweza kusingizia kuwa kuna vitu vimepotea na nilienda kwa mwenyekiti gharama ni kubwa kwa kweli mpaka nahisi napigwa

Je, watalamu wa sheria ni wakati gani sahihi wa Mwenye nyumba kuchukua hatua ya kuvunja na kumpangisha mtu mwingine na akawa yupo sahihi kisheria?

Asanteni kwa ushirikiano
 
Nenda kwa mtendaji atakuandikia barua unaenda nayo mahakama ya mwanzo wanakuandikia barua ya kuvunja hapo ukiwa na balozi na mwenyekiti wako wa mtaa, mwenyekiti ataandika Kila kilichopo ndani na nalala anabaki nayo yeye ila kumbuka wajibu wa kutunza hivo vitu unakua nao wewe, jiandae kua na stoo!

Ishanitokea hii nikafanya ivo
 
Nenda mbele zaidi mkuu mwambie huyo mtendaji akupe barua ya kwenda mahakama ya mwanzo...
Baadhi ya wapangaji ni vimeo Sana Mimi mwenyewe Nina mpangaji mmoja nimempangisha chumba na choo ndani,sebule nimemfungia na UMEME wake na meter ya maji anajitegemea lkn kwenye malipo Hadi nimkumbushe Hadi naona KERO..

Wapangaji wengine wako poa Sana na wengine ni michongoma
 
Fanya walivyoshauri wadau
Ila nataka kujua je huyo Mpangaji akirudi atawajibika kulipa gharama za usumbufu aloupata mpangishaji?
 
Nenda kwa mtendaji atakuandikia barua unaenda nayo mahakama ya mwanzo wanakuandikia barua ya kuvunja hapo ukiwa na balozi na mwenyekiti wako wa mtaa, mwenyekiti ataandika Kila kilichopo ndani na nalala anabaki nayo yeye ila kumbuka wajibu wa kutunza hivo vitu unakua nao wewe, jiandae kua na stoo!

Ishanitokea hii nikafanya ivo
Hata Mimi ilinikuta kesi kama hiyo mkuu, nimehangaika sana, siku tunavunja tukakuta kaacha makorokoro ya ovyo tu,
Nayo pia ikabidi niyahifadhi muda mrefu hata hakutokea kuyachukua,

Yule kijana mshenzi sana, Yani ukimwona humdhanii kabisa,
 
Nenda kwa mtendaji atakuandikia barua unaenda nayo mahakama ya mwanzo wanakuandikia barua ya kuvunja hapo ukiwa na balozi na mwenyekiti wako wa mtaa, mwenyekiti ataandika Kila kilichopo ndani na nalala anabaki nayo yeye ila kumbuka wajibu wa kutunza hivo vitu unakua nao wewe, jiandae kua na stoo!

Ishanitokea hii nikafany
 
Nenda mbele zaidi mkuu mwambie huyo mtendaji akupe barua ya kwenda mahakama ya mwanzo...
Baadhi ya wapangaji ni vimeo Sana Mimi mwenyewe Nina mpangaji mmoja nimempangisha chumba na choo ndani,sebule nimemfungia na UMEME wake na meter ya maji anajitegemea lkn kwenye malipo Hadi nimkumbushe Hadi naona KERO..

Wapangaji wengine wako poa Sana na wengine ni michongo

Nenda mbele zaidi mkuu mwambie huyo mtendaji akupe barua ya kwenda mahakama ya mwanzo...
Baadhi ya wapangaji ni vimeo Sana Mimi mwenyewe Nina mpangaji mmoja nimempangisha chumba na choo ndani,sebule nimemfungia na UMEME wake na meter ya maji anajitegemea lkn kwenye malipo Hadi nimkumbushe Hadi naona KERO..

Wapangaji wengine wako poa Sana na wengine ni michongoma
Duuh hatari Ndugu na alitakiwa aondoke free ila anataka kukomoa
 
Habarini za uzima ndugu zangu

Husika na kichwa cha habari hapo juu, naomba Niende moja kwa moja kwenye mada nilikua na mpangaji ambae alilipa pesa ya kodi yake vizuri wakati anaingia shida ni pale tu ilipoisha hakuweza Kulipa tena nikampa notice ya kuhama free bila kunilipa chochote ila huu ni mwezi wa tatu tangu amefunga kufuli lake kwenye chumba changu

Sasa naomba kufahamu najua anaweza kuwa ametega tukibomoa tu atataka kulipwa maana anaweza kusingizia kuwa kuna vitu vimepotea na nilienda kwa mwenyekiti gharama ni kubwa kwa kweli mpaka nahisi napigwa

Je, watalamu wa sheria ni wakati gani sahihi wa Mwenye nyumba kuchukua hatua ya kuvunja na kumpangisha mtu mwingine na akawa yupo sahihi kisheria?

Asanteni kwa ushirikiano
Kama mkataba wake umekwisha na haja renew, huyo sasa anahesabika kama mvamizi, fungua chumba chako endelea na mambo yako!!
 
Back
Top Bottom