Ibara ya 129 -(1): Wananchi watakuwa na haki ya kumuondoa Mbunge wao madarakani, endapo Mbunge atafanya moja wapo au zaidi ya mambo yafuatayo:
(a) Ataunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na maslahi ya wapiga kura au kinyume na maslahi ya Taifa;
(b) Atashindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapiga kura wake;
(c) Ataacha kuishi au kuhamisha makaazi yake kutoka eneo la Jimbo la Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi; au wapiga kura kumwajibisha Mbunge.
(d) Na kufanya mambo mengine yote yatakayoainishwa kwenye sheria ya nchi.