Haki yangu nitaipataje hapa?

enstein1

Member
Joined
Jul 14, 2009
Posts
68
Reaction score
29
Waungwana,
Nilisaini mkataba wa maandishi kupangisha nyumba hapa Arusha mwezi wa March, 2013; kwa miezi sita (marh - september) 2,100,000 bahati mbaya siku chache kabla ya kuhamia nikahamishwa kikazi.
Nikawasiliana na mwenye nyumba akadai pesa kishaitumia.
Tukakubaliana nimrudishie funguo dalali wake ili akipatikana mtu nirudishiwe pesa yangu. Tumekuwa tukiwasiliana mara kwa mara na jibu lilikuwa hajapata mtu.
Desemba hii nilitakiwa kurudi Arusha, nikamuuliza mwenye nyumba juu ya kuipata nyumba ile akanambia alishapata mtu! Kumuuliza juu ya makubaliano yetu kaanza kunipa majibu ya kukstisha tamaa! Mara anadai mkataba wangu ulishaisha; mara c wajibu wake kulipa sababu c yeye aliyezuia mimi kuhamia!? Nahic ananiruka!
Nitafuatiliaje suala hili kisheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…