Haki za binaadam walivyo waharibu wanafunzi mashuleni

Yasser5

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2012
Posts
207
Reaction score
17
Ni kweri dunia imebadirika lkn mabadiliko hayo yasipo zingati mfumo mzima wa maisha yetu mwisho wa siku atakosena nani wa kulaumiwa means too lait

Nakumbuka zamani mim nilikuwa nikibishana na kaka yangu au dada yangu mkubwa kama baba akiniona mim ndo nachapwa bila kuangalia nani kaanza kwa mantiki ya kwamba mkubwa aheshimiwe na mwisho wa siku heshima ina rudi na hamna majadiliano ya kwa nin nimeadhibiwa means i cnt question dudy siku hiyo inakuwa imekula kwangu

leo nimeshuhudia baba mmoja akitoka kazini kisa mtoto kachapwa shuleni baba anaenda shuleni kulianzisha
haki za binadam mnatupeleka wapi tuna zalisha watoto na taifa lenye nidham gani?
 
Shule za Tanzania kweli zimezidi sana kuwaadhibu watoto wadogo kwa kuwachapa na kuwapa adhabu kali sana, kuna shule moja huko mkoa wa singida watoto walikuwa wanakandamiziwa mikono yao katika miba (Kosa eti hawakufanya vizuri home work). Pia kuna shule ingine huko Igunga mwalimu alikuwa anawachapa watoto mpaka wanachanika ****** yao.

Walimu kama hawa lazima wastomishwe na wahukumiwe lazivyo wataharibu akili za watoto, ndio maana Tanzania haina maendeleo yeyote (watoto wanaharibiwa akili zao tokea shule ya vidudu).

Mtoto anapigwa vibaya sana na hali bado yupo shule ya vidudu (chipukizi)!!! Inasikitisha sana.
 
kweri=kweli
dudy= dady?
Badirika=badilika
mashureni=mashuleni
lait=late?

Ndo utandawazi huo...wengine wanapohamasisha kupigwa marufuku viboko wanapata ulaji. Ingawa kwa case hiyo sidhani kama wanaharakati wana la kulaumiwa, mzazi mtoto ameadhibiwa badala ya kumshukuru mwl unaenda kumkaripia mwalimu? Hapo kosa la mzazi, enzi zetu ukicharazwa bakora shule huthubutu kusema nyumbani maana utaongezewa mikwaju, unless mwalimu amekupiga kupitiliza...
 

BADILI TABIA hivyo hivyo husiache kufanya masahihisho kama hayo hapo juu, itafika kipindi sasa irabu hazitumiki tena.Hongera sana nap pia hata kama ni mimi usiache kunisahihisha..SORY KWA KUBADILISHA MADA ILA NDIO JF!
 

BADILI TABIA hivyo hivyo husiache kufanya masahihisho kama hayo hapo juu, itafika kipindi sasa irabu hazitumiki tena.Hongera sana nap pia hata kama ni mimi usiache kunisahihisha..SORY KWA KUBADILISHA MADA ILA NDIO JF!
 

unatakiwa uwe na uhakika ya uyasemayo sio kusimuliwa juzi tu hapa nimeshuhudia mtoto kachapwa viboko viwili kwa fimbo ya kawaida yeye kakimbia kuleta mzazi eti kachapwa na mwiba wazazi wasipokuwa waangalifu watapoteza mwelekeo wa watoto wao.mzazi akiitwa kuangalia maendeleo ya mtoto wake shule anasema yupo busy itokee mtoto kachapwa ubusy unaisha sasa tunazalisha taifa lipi?
 
Wakuu, mazingira ya kwetu ni tofauti mno na mataifa yaliyoendelea. Asilimia kubwa ya watoto wetu hulelewa na mitaa. Halafu tunataka wawe na tabia za watoto waliolelewa na wazazi! Kwetu sisi bakora ni must.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…