Kaka swali lako refu itabidi uende kwenye sheria zinazohusu mambo ya upangishaji. Lakini kwa kifupi ninazozikumbuka ni zifuatazo:-
Haki za mwenye nyumba:
Kulipwa kodi yake kutokana na mkataba unavyosema baina yenu, kuingia na kukagua nyumba kwa ruhsa ya mpangaji,
Wajibu wa mwenye nyumba: Ni kuhakikisha nyumba anayopangisha ni nyumba ambayo inafaa kukalika, mfano ina choo iko katika hali nzuri sio imebomoka kiasi haifai kukaliwa na binadamu, wajibu wa kufanya matengenezo makubwa katika nyumba kama ktk mkataba hamkukubaliana kuwa itakuwa matengenezo ya mpangaji, wajibu wa kulipia kodi za serikali za nyumba hiyo kama haiko katika makubaliano na mpangaji, Biashara utakayofanya iwe ambayo mmekubaliana na mwenye nyumba wakati unapanga ukibadilisha kama hatoridhika nayo ana haki ya kusitisha mkataba wako mf. Umepanga ili uendesha duka la vifaa vya shule, mara umebadilisha unaweka baa ya kunywa pombe za kienyeji na unasababisha wapangaji wengine wenye biashara zao kutoridhika na biashara hiyo mpya.
Haki za mpangaji:
Kuishi katika nyumba aliyopanga bila kubugudhiwa na mwenye nyumba,
Wajibu wa mpangaji:
Kulipa kodi kama walivyokubaliana na mwenye nyumba, kuishi katika nyumba anayokaa bila kuichafua kiasi cha kufanya hiyo nyumba isikalike na mtu mwingine, kutopangisha mpangaji mwingine bila makubaliano maalum na mwenye nyumba akiondoka, kulipia matumizi mbali mbali ya umeme na maji, simu kama vitu hivyo vipo na havikuainishwa kwenye mkataba kuwa viko katika kodi, wajibu wa kutobadilisha sura ya jengo alilopanga bila idhini ya mwenye nyumba na akiondoka hatakiwi kubomoa kiasi cha kuharibu jengo aliloliacha, wajibu wa kuhakikisha unachokifanya hakiwaudhi wapangaji wengine, wajibu wa kulipia kodi za serikali za biashara unayoifanyia hapo mahali.
Serikali inaruhusu nyumba yeyote bora iwe na huduma muhimu za binadamu kama maji, choo, na mazingira masafi ya kufanyia biashara. Lakini pia eneo hilo liwe limeruhusiwa kwa biashara hiyo unayoifanya. Mf. huwezi kuweka baa eneo la shule ni makosa. Au ukaweka kituo cha kuuzia mafuta wakati watu wanaishi kwenye nyumba hiyo hiyo au kiwanda ukajenga sehemu ambayo imetengwa kwa ajili ya mambo mengine.
Malipo ni makubaliano ya mwenye nyumba na mpangaji. Lakini vigezo vifuatavyo ndio vya kuzingatia. Jinsi ya kulipa kodi - kwa siku, wiki, mwezi au mwaka n.k., au malipo kwa ukubwa wa eneo, mita za mraba, kwa chumba nk.
Kila la kheri