haki za mlaji "consumer's rights"

Voice of Wisdom

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
537
Reaction score
240
habari za asubuhi wakuu, kama kichwa cha mada kinavyojieleza, Tanzania tumekuwa tukishuhudia ukiukwaji wa haki za mlaji katika maeneo mbalimbali.
Kwa sasa kuna jumbe za simu zinawafikia watumiaji wa voda(mitandao mingine sijui)kutoka clouds tv bila kujali kwamba umejiunga na hiyo huduma au la!
Binafsi ni mhanga wa hii kadhia wanakutumia sms za fiesta hata kama hujajiunga na kibaya zaidi kila sms wanakukata salio la tsh 100. Nimewapigia voda huduma kwa wateja wanadai hawahusiki ila cloudstv ndio wamefanya hvyo(kutuunganisha na hiyo huduma ya fiesta sms)
Wanasheria mlioko humu ndani naomba mtusaidie kwani kwa maelezo ya mtoa huduma kwa wateja tatizo ni kubwa!
Fikiria kuwa kuna wateja 500,000 wanaotumiwa hizi sms bila idhini yao kila siku kwa muda wa wiki 1 ni kiasi gani tutakuwa tumeibiwa kama watanzania walala/waamkahoi(500,000x100x7=350,000,000/)
Je huu si wizi kama ulivyo wizi mwingine?
Tcra naamini pia mpo huku, tunaomba msaada wenu..
Maeneo haki za mlaji zinapovunjwa ni mengi sana na hakuna anayejali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…