Haki za raia katika tume ya Warioba zisipuuzwe

Haki za raia katika tume ya Warioba zisipuuzwe

tpmazembe

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
2,469
Reaction score
586
Tumekuwa tukipata malalamiko makubwa sana hasa kwa wananchi wa tanganyika waishio zanzibar, kwamba kuonekana sio raia na kubaguliwa.

Kama ccm wanania njema na muungano huu ,walete serikali zozote lakini haki za raia katka tume ya warioba ziwepo.

kama watanganyika wataendelea kuishi kama watumwa wanapokuwa visiwani,hali hiyo ni mbaya na italeta machafuko makubwa baadae.

Ni bora muungano kama haki hizo haziwezekani kuwepo kwa raia wote ndani ya muungano.basi muungano huu uvunjike,maana hauna faida yeyote zaidi ya kugeuza wananchi wa upande mmoja kuwa watumwa upande wa pili na kuonekana kama wanajipendekeza.

Narudia tena kama haki hizo zitapuuzwa ni bora tusiwe na muungano,maana hautakuwa muungano wa wananchi wa pande zote bali wa wanasiasa kugawana mafungu ya kodi za wananchi.huku wananchi wakiendelea kuishi kama watumwa ndani ya nchi yao.
 
Back
Top Bottom