kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Kwa ufupi
"Hayo yalisemwa na Katibu wa kundi namba nne, Leokadia Vedastus huku akitaka katiba hiyo ijayo iongeze wigo wa haki za mfanyakazi ili aweze kulindwakikatiba."
Ukerewe. Wajumbe Baraza la Katiba Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, wamependekeza haki za wafanyakazi zitazamwe upya kwenye Katiba ijayo.
Hayo yalisemwa na Katibu wa kundi namba nne, Leokadia Vedastus huku akitaka katiba hiyo ijayo iongeze wigo wa haki za mfanyakazi ili aweze kulindwakikatiba.
Vedastus, alisema wamependekeza wigo wa haki za wafanyakazi uongezwe kwenye katiba kwa kutambua kuwa katiba ndio sheria mama ya nchi na sheria zote zinawajibika kwenye katiba hiyo.
Alisisitiza kuwa kwa haki hizo kuwepo kwenye Katiba kutaweza kumwongezea ulinzi mfanyakazi hivyo kuwafanya waweze kufanya kazi katika mazingira bora.
Alisema kwa muda mrefu haki nyingi za wafanyakazi zimekuwa hazitambuliki kikatiba hivyo kusababisha wafanyakazi wengi kunyimwa haki zao.
Katiba Mpya ina wajibu wa kuongeza wigo wa haki za wafanyakazi, siyo kuishia kuwekahaki ya kufanya kazi pekee yake bila kuambatanisha haki zingine,alisema Vedastus.
Chanzo: MWANANCHI