Hakika Lowassa alionewa katika hili tukio kubwa la kihistoria lililotokea mwaka 2008

Hakika Lowassa alionewa katika hili tukio kubwa la kihistoria lililotokea mwaka 2008

Matukuta Jr

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
207
Reaction score
27
''Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe ni mwanasheria, alikuwa anafundisha wanafunzi Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni 'NATURAL JUSTICE'.

Mheshimiwa Spika,

Wewe pia ni mwanasheria unafahamu suala la 'NATURAL JUSTICE'. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani. Wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi,lakini mimi ambaye ni mmoja katika watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.

Mheshimiwa Spika,

Nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu (Dar es Salaam) hata wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.

Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya 'oversight' kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja
walizojenga wamesema 'Waziri Mkuu ilikuwa hivi'.

Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza 'Waziri Mkuu wanasema ulitoa dokezo hili ni sawa sawa ni kweli'? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westmister kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.

Mheshimiwa Spika,

Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki hakitaonekana kutendeka haki nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia.

Kwa hiyo, nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba, naona si sahihi, NIMEFADHAIKA SANA, NIMEDHALILISHWA SANA, NIMEONEWA SANA KATIKA HILI. Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani ya kuniuliza,kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo zangu?

SISI WOTE HAPA NI WANASIASA, TUKIANZA KUAMINI MINONG'ONO YA MITAANI NIAMBIENI MWANASIASA ATAKAYESIMAMA. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Mheshimiwa Spika,

Lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikuwa na ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka kwa Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika,

Naamini ingekuwa ni heshima kubwa wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo
imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa Spika,

Lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi hasa kulikoni mpaka watu wazima, wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo, kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.

Mheshimiwa Spika,

Nimetafakari sana kwa NIABA YA CHAMA CHANGU, KWA NIABA YA SERIKALI YANGU nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha DHANA YA UWAJIBIKAJI lakini na KUTOKUBALIANA NA UTARATIBU ULIOTUMIKA KUSEMA UONGO NDANI YA BUNGE WA KUMSINGIZIA MTU.

Edward Lowassa (MP),
Rtd PM
 
Hebu tuangalie kwanza maelezo ya lowasa



...hatupaswi kushabikia mambo makuu yanayohusu uendeshaji wa nchi Kama kushabikia clab Za mpira. Maelezo ya mh. Lowasa yanaonyesha kua yeye Ni Mtendaji asiesita . Tukumbuke kua Lowasa analaumiwa Kwa Sababu ya jitihada zake ktk kutatua tatizo la umeme. Ushahidi kua alifuata taratibu zote Na kwamba alishinikizwa kujiuzulu kinyume kabisa Cha haki Ni kua serekali inalazimika kuwalipa dowansi mabilioni.

Ingekua Dowansi Ni kampuni Hewa iliyoingia kazini bila kufuata taratibu isingeweza kushinda kesi kila mahakama.

Unapomtaja Lowasa unalazimika kuona kasi ya maendeleo ktk kipindi chake kifupi. Mradi mkubwa wa Maji ziwa Victoria , ujenzi wa kasi ya ajabu wa sekondari nchi , Ujenzi wa kutisha wa chuo kikuu Dodoma. Kwa kweli hata aliweka nidhamu kubwa ktk watendaji Na matumizi ya serekali.

Hakika sioni mtu mwingine Tanzania Mwenye ushahidi wa utendaji unaolingana Na Mh. Lowasa.

Lowasa Ni jembe, we acha tu.......
 
Last edited by a moderator:
Tulioonewa ktk sakata hili ni sisi wavujajasho na walipakodi wa Tz, hamna victim mwingine ktk haya yote..tuache upumbavu/
 
yaani unataka kuniambia lowasa ndiye aliyebuni mradi mkubwa wa maji ziwa victoria,shule za kata na ujenzi wa udom????
 
Back
Top Bottom