Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,746
Hatimaye nimepata Takwimu mpya za Elimu kwa mwaka 2009. Haijawahi kutokea katika historia ya Tanzania wanafunzi kuingia Sekondari kwa wingi kama wakati wa kipindi cha Edward Lowassa. Historia itamsuta kwa mengi lakini kwa hilo jamani tumpe hongera yake. Hongera Edward Lowassa!
Ni kweli kwa ujumla shule za Kata ni za kiwango cha chini hasa ukizingatia kuwa kwa kiasi kikubwa zinaendeshwa na Walimu wa Vodafasta. Ndio, wanafunzi wa shule hizo wanakaa kwenye ndoo kama walivyopigwa picha kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti la Mwananchi la leo. Naam ni kweli kabisa kuwa wananchi waliburuzwa sana tu ili wajenga shule za Sekondari.
Pamoja na hayo yote ni heri mwanafunzi akae chini shuleni kuliko kukaa tu nyumbani. Pia ni heri tushughulikie suala la ubora wa elimu wakati wanafunzi wako tayari mashuleni kulikuwa kulishughulikia wakati wanazagaa mitaani. Pasipo na mori wa Kilowassa na Kisokoine hatutaweza kuendeleza sekta hii ambayo ndio msingi mkuu wa kuwatokomeza wale maadui wanne wa maendeleo: Umaskini, Ujinga, Maradhi na Ufisadi (Hilo la nne sijaliongeza mimi, aliliongeza Mwalimu Nyerere mwenyewe kwenye Hotuba zake za miaka hiyo - kama mnataka rejea nitawatumia hivi punde!)

Mkuu mbona ujaacha kuboronga. Kuanzisha ni kitu rahisi sana kuliko kuendeleza.
Alichofanya Lowassa sio kitu kipya Tanzania. Lakini matatizo yake ni kuviendeleza shule hizo. Hakuna sustainability yoyote ambayo itafanya shule hizo kutoa watoto wenye elimu ambayo itawafanya kuboresha mazingira yao.
Nyerere alianza na elimu ya UPE mpaka leo ubora haujaongezeka. Sasa kwanini tufikiri kuwa mipango ya Lowassa itafanikiwa.
Robert alijenga secondary kila kata mara baada ya uhuru. Na mpaka wa sasa wana struggle.
Siku zote usipunguze standards hili kuongeza quantity.
Kumbuka hata Mtoza Ushuru Zakayo alirudisha mara dufu ya dufu mali alizowadhulumu wananchi wa enzi hizo na Masihi akamwezesha aanze upya mbele ya kadamnasi - Hakika ile ziara ya Lowassa kule kwenye 'Nchi Takatifu' huenda ilimbadilisha na akazaliwa upya kama Saulo wa Taso, tumpe nafasi tena tuone jinsi elimu yetu itakavyopaa na kutuwezesha kufikia malengo ya milenia kabla ya 2015!
Mchungaji Kishoka u wapi, shusha sala ya ubatizo tuanze upya na Edo wetu!
Nafikiri Sala ya Utakaso ingefaa zaidi.Kwa maoni yangu huyu jamaa hata mngemzamisha kwenye kijito cha utakaso halafu mkamuosha kwa Hisopo hakika hawezi kuwa safi tena.
Sasa ataendeleza vipi na ninyi mlikuwa "mnautaka Uwaziri Mkuu" na mkauchukua kisha suala la Richmond mkaligwaya baada ya kuupata!
Tatizo lako hujawahi kupata njaa kama ile ya wakati wa Ukame wa Sahell!
Huyu bwana kweli ana bahati! kwa maovu hayo bado kuna watu wanamhitaji!!! Mungu tusaidie sisi bado vipofu.
mbona hamzungumzii mvua ya kutengeneza kutokea thailand?? oh...aliingiza wananfunzi wengi.......nyoo......hiyo mvua ilikuwa......hee richmonduli2. Hakika ukizoea kuiba unaiba hadi maiti ukidhani inauzika, we hata wazungu tunaoamini wana pesa na akili hawaja fikiria mvua ya kutengeneza .....lowasa na mvi zake anakurupuka na mvua ya kutengeneza!!!!!mwe...twafwa twilola.
Mkuu uliyoyanena hayapingiki. Ila lazima tujiulize iweje Baba wa Kambo anashindwa, hata maziwa ya mgando hatupi! Takwimu zimeanguka vibaya sana toka tumweke benchi Baba Edo aliyewahi kughani 'Tupo Tumejaa Tele'! Sasa mbona wenzake aliowaacha hawapo tena wala hawajajaa tele?