MJUMBE WA NCHI
Member
- Jan 2, 2015
- 53
- 23
Imesemwa sana na wengi kuwa ccm hawana nia ya kutupatia wananchi katiba bora lakini nilikuwa sielewi vizuri.lakini nimeshuhudia nakuelewa wakati zilipoanza kusambazwa nakala za katiba pendekezwa.katika wilaya yetu zilipofika hizo nakala kamati kuu ya ccm wilaya ilikaa kikao agenda kuu ni namna ya kuipigia kura ya ndiyo katiba pendekezwa.iliamriwa kila mtendaji wa kata,kijiji,wakuu wa mitaa na vitongoji kuhakikisha wanashawishi wananchi kuikubali katiba pendekezwa.mjumbe mmoja alisema "katiba hii ni yetu lazima tuisimamie ipite" tarehe 27 katika kata yetu kilifanyika kikao cha w.d.c ambacho kilitoa maagizo ya kuwa kila mjumbe ahakikishe anahamasisha wananch kuikubali katiba pendekezwa.hii ni hila ya kwanza niliyoiona.hila ya pili ni usambazaji wa nakala zenyewe:kata yetu inakaya 3000 lakini ilipewa nakala 300,ukigawa 3000 kwa 300 utaona kuwa kaya 10 zote zinachangia nakala moja wakati muda wa kuzisoma nakala umebaki wiki mbili tu.hapa lengo wananch wasisome katiba hyo pendekezwa ili wasijewakajua wakaamka.