Ndugu zangu wanaJF haswa sisi tuliobahatika kupata Loan kutoka heslb, hakika twapaswa kumshukuru mungu na si majivuno ukizingatia kuna wenzetu wamekosa, tena mimi ni mfano wa waliochaguliwa course zisizo na kipaumbele na tumebahatika kupata mikopo.
JF Imekua msaada kwangu toka nilipojiunga nikiwa ndio naingia form 6 na nimejifunza mengi kutoka wa wanachama na shukrani maalumu nazipeleka kwa bwana
Maganga Mkweli jamaa amekua msaada kwangu toka tarehe 1 mwezi wa 5 yalipotoka matokeo ya kidato cha sita, amenishauri, uchaguzi wa vyuo, uchaguzi wa course hadi namna ya kujaza form za heslb na hatimae nimefanikiwa ingewezeka ningeleta PM zote hapa kama ushahidi lakini sheria za JF haziruhusu.
Ningeweza hata kumtumia japo ka-elfu ishirini anunulie vocha lakini nimeamua kuchangia JF pindi nitakapo pata boom ingawa nimeambiwa pesa zile si nyingi lakini nitapiga Lampard, 101 ili mradi nitimize ahadi yangu.
Nawashauri na wenzangu mwaweza kuchukua hata kiasi kidogo cha boom mkaichangia JF ili majukwaa haya yaje kuwasaidia wadogo zetu ikiwezekana watoto zetu.
Ahsanteni, kwa kuniunga mkono.
Ipycalypse.