Utangulizi: USHAIRI
1. Nimesimama pekeangu, kutetea jamii yangu,
Mimi na vijana wenzangu, hatuoni mwisho wetu,
Wingu limejaa ukungu, macho yamekua vipofu,
Hivi ni kweli hamtuoni, au mmevaa miwani.
2. Sio wali sio ugali, vyote havipiti kooni,
Hayo mashati na suruali, hazikai kiunoni,
Mmenitupa hamnijali, sisikii hata honi,
Basi ninagonga hodi, naombeni nifungulieni.
3. Nimekuja na maswali, majibu yake yapo wazi,
Ila mlivyo janjari, hamtaliweka wazi,
Nimekoswa na ajali, ili nifike uswazi,
Hakika uswazini kwetu, ni zaidi ya ugali.
4. Niambie nielewe, msiniache taabani,
Bora mniache nilewe, msinitupe msituni,
Usije ukawa mwewe, kifaranga unirubuni,
Uswazi wa kwa jirani, sio kama wa nyumbani.
5. Mmetuletea tenki, ili tuyapate maji,
Wala hili sio feki, lakini halina maji,
Matumizi yake feki, kuliona sitamani,
Miaka miwili ya haki, na maji hatuyapati.
KIINI;
Kiuhalisia, mshairi ana maumivu ambayo yanahitaji tiba. Madaktari wakuu wapo wa kutosha na waliobobea lakini tatizo ni wasaidizi wao, wanawanyonya wagonjwa kiasi ambacho mpaka mgonjwa kufika kwa daktari bingwa anakua na hali mbaya katika dakika za majeruhi.
Ili Tanzania Tuitakayo isifanane na hii ya sasa lazima mapengo yote yazibwe, na wagonjwa wahudumiwe kwa haki stahiki pasipo uwepo wa viti maalum. Labda ninatumia lugha fumbo ambayo inahitaji ufumbuzi, nianze kwa kuuliza, Je! Uongozi wa juu unafatilia utendaji kazi wa viongozi wa ngazi ya chini katika maeneo yao husika. Kama jibu ni ndiyo, kiongozi wa uswazini kwa mshairi, aseme ametekeleza vipi aliyoyaahidi wanauswazi. Kama ni hapana, tujue ni kwa nini hamfatilii.
Hii ndio sababu ya mshairi kusema kuwa ugali dagaa kwenye amani ni mtamu kuliko wali nyama vitani, Ila anaoula una uchungu wa ajabu. Tanzania Tuitakayo ili ifanikiwe ni lazima viongozi wote wawajibike kwa haki na usawa ili jamii itatue changamoto zao kupitia wao. Na kwa kufanya hivi tutamsaidia Rais wetu kuwa na majukumu machache. Ajabu ni napoona baadhi ya maeneo yanaendelea kiuchumi huku mengine yanasitasita kuendelea, nafikiri ni kutokana na uongozi wa sehemu husika.
Miaka 5, 10 na 25 ijayo Tanzania Itakua sawasawa na tunayoitaka ikiwa changamoto za sasa zitatafutiwa utatuzu ili zisiwe sehemu ya maisha ya kila siku kwa mtanzania.
Uswazi kwa mshairi kuna changamoto ya huduma ya kijamii, maji yamekua ugonjwa ambao mpaka hivi sasa naandika haya mgonjwa hajamuona daktari bingwa. Eneo la Kinyerezi, Mongo la ndege ni mfano mzuri kwa uswazi wa mshairi, ni miaka zaidi ya mitatu Matank yaliyowekwa na serikali hayatumiki ipasavyo, watu wanataabika kuvuta maji kisimani na kununua maji ya watu binafsi ikiwa mabomba wanayo vibarazani mwao.
Viongozi wa ngazi zote kuanzia wajumbe, diwani na mbunge wote wapo na afya njema kabisa, lakini Hali ya wananchi wao katika hitaji muhimu la maji hawalitatui. Wenye pesa wanaagiza magari yawaletee maji kwenye mapipa yao, je mwenye hali ngumu Kama ya mshairi atajikwamuaje. Ikiwa tatizo hili Lina miaka zaidi ya mitatu, litashindwa kufika miaka 5, 10 na 25 ijayo. Serikali kuu itazame utendaji kazi wa uongozi wa chini na itoe maamuzi.
Katika sekta ya usafirishaji naipongeza serikali, kwani uswazini kwa mshairi kuna lami, hata kwa majirani zake. Lakini jirani wa kitunda mwanagati na kibeberu,ugali wake pia mchungu. Barabara ya mwanagati Ni njia fupi ya kutokea buza lakini kuifikia buza kunatumia muda mrefu kutokana na miundombinu hafifu. Barabara ya kutoka banana kuelekea kitunda imekua ikitengenezwa kwa kiwango Cha lami kwa miaka kadhaa lakini zoezi hilo linaishia Kati na liendelei tena, inapofika msimu wa mvua zinaharibika na ubovu wa barabara kuwa Kama zamani, Hali hii itaisha lini.
Zaidi ya miaka mitano wakazi wa kitunda na mwanagati hawana njia nzuri ya usafirishaji, Kama gonjwa hili halikutibiwa miaka 5 iliyopita litatibiwa kwa miaka 5, 10 na 25 ijayo. Barabara ya kitunda na mwanagati ni mfano tu, Ila barabara zinazohitaji kuwa katika kiwango zipo nyingi, ukifika mda wa kampeni tunaahidiwa mengi lakini dereva akishashika usukani safari inakua atakavyo.
Tunashukuru kwa ujio wa treni ya mwendokasi hakika ni mkombozi kwa wasafiri wa Morogoro. Changamoto ipo kwenye vivuko vya reli, magari yamejengewa barabara na waenda kwa miguu kupita kando yao kwa usalama kabisa, changamoto kuu kwa sasa ni kwa wananchi wanaotembea kwa miguu, inawalazimu kupita kwenye matundu ya mtaro chini ya reli ambayo si salama ili kufika kwa haraka ng'ambo ya pili ya reli kwani umbali wa kivuko kimoja kwenda kingine ni mkubwa sana. Hivyo inawalazimu kupita njia za hatari. Je! Serikali na viongozi wa maeneo husika wamejiandaaje kutatua changamoto hiyo. Nimeona niseme Leo huenda serikali itatambua changamoto hii, lakini tukiendelea kunyamaza serikali haitatambua ugumu tulionao.
Elimu ni ukombozi, ufunguo wa maisha, elimu ndio kila kitu. Wanafunzi wanapaswa wasome kwa furaha kuanzia kwenye mioyo yao ili wafaulu vizuri, lakini kwa baadhi ya wanafunzi makasiriko yanaanzia pale tu wanapoamka na kuondoa furaha yao. Wanaamka saa10 usiku kujiandaa kwenda shule ambazo zipo mbali sana na makazi yao, hivyo kuwapelekea kuchoka na kusinzia madarasani kwani kero ni nyingi, makondakta wanawakataza kupanda magari na wengine kusukumwa, hii inahatarisha usalama wao, Je! kwa changamoto hizi mwanafunzi amlaumu nani?
Mfano halisi ni Mwanafunzi mkazi wa Kinyerezi anafaulu darasa la saba, lakini shule anapangiwa Chanika mvuti, na wakati huo mwanafunzi wa mbondole anapangiwa Kivule, huku mwanafunzi mkazi wa ulongoni anapangiwa shule ya tabata, makazi ya wanafunzi na shule wanazopangiwa hayawiani kwa umbali. Jibu linalokuja pale unapouliza ni kwamba, kata husika haina shule ya sekondari ya serikali hivyo inategemea shule za kata zingine. Je! Viongozi wa kata ambazo zina shule za sekondari zaidi ya 5 wametofautiana nini na viongozi wa kata zenye shule 2, kwa nini na wao wasiwe na shule zaidi ya 5 ili kuchoche ufaulu kuanzia kwenye mazingira rafiki kwa wanafunzi? Wizara ya elimu isaidie kutatua changamoto hii kwani pasipo utatuzi hatutaweza kuipata Tanzania Tuitakayo miaka 5, na 25 ijayo.
Ikiwa magonjwa haya yatamfikia daktari bingwa Nina imani yatatibiwa na kutokomezwa kabisa, hivyo kuipata Tanzania Tuitakayo miaka zaidi ya 5,10 na 25 Tunayoitazamia.
Nasisitiza kuwa ili ugali uwe mtamu kwenye amani, lazima viongozi wote wawajibike kwa haki na usawa. Kwa kufanya hivyo Tanzania Tuitakayo itakuja bila kutafutwa na ndipo tutakapokula wali nyama kwenye amani na utulivu.
Nina mengi ya kusema Ila naomba niishie hapa, Asante.

Upvote
2