Hakika utachoka kama umeamua kufanya kazi ya kumridhisha mwanadamu

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara - 36:
Hakuna kitu ambacho kinaweza kumridhisha au kumtosheleza mwanadamu wakati wote. Si pesa wala kitu chochote cha thamani. Kitu pekee anachoridhika nacho mwanadamu ni kifo chake.

Mwanadamu haridhiki wala hatosheki. Kama shughuli zako unazofanya kila siku zinahusiana na kuwaongoza watu au kuongoza kampuni yenye watu kamwe usihangaike sana kutaka kuwaridhisha na kuwatosheleza wafanyakazi wako, ukifanya hivyo uitazika kampuni.

Mwanadamu anaweza akawa anachukia kwenda kazini - kazi ambayo aliiomba yeye mwenyewe. Na hata kama utampa ofa ya kumpunzisha kwa mwaka mzima huku ukimlipa stahiki zake zote bado atakulalamikia.

Fanya kwa kiasi huku ukijua kuwa huwezi kumridhisha mwanadamu. Kama unadhani ukimnunulia mpenzi wako gari zuri ndo ataridhika, bila shaka anaweza kukusaliti kwa mtu ambaye alimwekea mafuta ya Tsh elfu kumi.​

Right Marker
Dar es salaam.
 
Wanaume ni wabaya, wanawake ni waovu
 
Back
Top Bottom