Hakikisha unapokatishwa tamaa haukati tamaa mpaka mkatisha tamaa akate tamaa ya kukukatisha tamaa

Joined
May 2, 2018
Posts
20
Reaction score
27
Coach Lazaro Samwel:
*#AchaNikufungue@2018*

Tip No. 10

" Hakikisha unapokatishwa tamaa haukati tamaa mpaka mkatisha tamaa akate tamaa ya kukukatisha tamaa. Ukishindwa hili funga ndoa na kusonga mbele alafu iache tamaa ikatee tamaa nawe." - mgambilwa
Muda ambao wengine wanakuona kwamba umechanganyiwa kwa kitu ambacho umeamua kukifanya kisa tu hawajawahi kukiona au kukisikia kwa watu wengine ndio muda wa kukaza zaidi katika jambo lako, kwasababu kushangaa kwao na kukupinga kwao ni fursa tosha ya wewe kuwa tajiri pale tuu utakapokamilisha kile ambacho kinafanya wewe kuonekana mjinga au huna akili.

Cha msingi zaidi kumbuka pia muda ambao unawaza kuacha kile kitu muhimu unachofanya kwa wengine ndio muda ambao unatakiwa kuongeza upya hari ya kukifanya unachokifanya tena kwa ubora zaidi ya mara ya kwanza kwasababu huko ndipo penye ubora ambao unatafutwa lakini haujapatikana kwa kuwa wengi huishia njiani kwa maneno ya watu au kwa kukatishwa tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…