Hakimu aliyedaiwa kupokea rushwa hana kesi ya kujibu

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2009
Posts
3,517
Reaction score
1,363
[h=2]
[/h]



Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Pamela Kalala


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Pamela Kalala, aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kuomba na kupokea rushwa ya Sh. milioni tatu.

Akitoa Hukumu hiyo jana Hakimu Aloyce Katemana, aliiambia mahakama kuwa ushahidi uliopelekwa mahakamani dhidi ya mshtakiwa umeonyesha kuwa hana kesi ya kujibu na hautoshi kumtia hatiani.

Hakimu Katemana alisema inaonekana Hakimu alimfutia mshtakiwa, dhamana bila sababu na alifanya uzembe kufuta bila kuweka kumbukumbu na siyo rushwa kama inavyodai kesi hiyo.

Pia alisema hakuna mtego wowote unaoonyesha mshtakiwa alipokea rushwa. Shahidi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), alidai mahakamani kuwa alipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa mshtakiwa alipokea 100,000 kwa njia ya Tigo Pesa.

Ila kwa mujibu wa taarifa hizo siyo mke wa mshtakiwa aliyemtumia pesa hizo bali zilitumwa na wakala.

Aliendelea kusema kuwa ushahidi unaonyesha mke wa mshtakiwa hakulalamika mahakamani ila alilalamika kwa Msajili wa Wilaya, Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam.

Alisema katika barua Josephine Wage alilalamika kwa msajili kwamba hakimu hakutenda haki na siyo amepokea rushwa.

Hakimu Katemana alisema mshtakiwa hana kesi ya kujibu kulingana na mashtaka yanayomkabili ya kuomba na kupokea rushwa.

Upande wa Jamhuri, uliongozwa na Wakili wa Takukuru, Sophia Gura na ulileta mashahidi saba.

Kwa mara ya kwanza Kalala alifikishwa mahakamani hapo Septemba 24, mwaka jana akidaiwa kuwa katika tarehe tofauti Februari mwaka huu jijini Dar es Salaam aliomba rushwa ya Sh. milioni tatu kutoka kwa Josephine Wage, ambaye ni mke wa mmoja wa washtakiwa wa kesi ya jinai namba 703 ya mwaka 2008.

Kesi hiyo ni ya Jamhuri dhidi ya Abubakari Mziray na wenzake ambayo mshtakiwa aliomba fedha hizo ili iwe kishawishi cha kutoa upendeleo kwa mume wa Josephine Wage, wakati wa kutoa uamuzi.

Kosa la pili ilidaiwa kuwa, katika tarehe zisizofahamika, Februari mwaka huu, mshtakiwa akiwa kama Hakimu Mkazi na wakala wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kinyume cha kifungu namba 11/2007 cha sheria ya Takukuru alipokea rushwa ya Sh. 800,000 kutoka kwa Wage.

Kosa la tatu, ilidaiwa Februari 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alipokea rushwa Sh. 100,000 kutoka kwa Josephine Wage ili iwe kishawishi cha kutoa upendeleo kwa mumewe wakati wa kutoa uamuzi katika kesi inayomkabili.
 
naona huyu hakimu Katemana hakuwa likizo kwa kesi hii kama ilivyokuwa kwa Ndugu Lwakatare
 

Kwa mara ya kwanza Kalala alifikishwa mahakamani hapo Septemb
a 24, mwaka jana akidaiwa kuwa katika tarehe tofauti Februari mwaka huu jijini Dar es Salaam aliomba rushwa
Mahakama ikiamua inaweza, septemba 24 leo kesi imekwisha, it goes in the books of history as the fastest case ever
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…