Hakuna Atakayesimama Mbele Yetu.

Joined
Sep 10, 2018
Posts
7
Reaction score
3
Neno la Mungu linasema katika Yoshua 1:5 Hapatakuwa na mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.

Mungu wetu ni mwema na mwaminifu sana kwa watu waliowema na waaminifu kwake. Vitu gani vinatuzuia ni magonjwa au umasikini au ugumba au, kutokuwa na ndoa au kazi au ni watu gani wanaosimama kuzuia baraka zetu. HAKUNA kabisa tukiwa tunamtegemea MUNGU katika maisha yetu na kumsikiliza Roho Mtakatifu, vyote tunavyovihitaji katika maisha yetu tutavipata kwa sababu Mungu anaona na anajuwa mahitaji yetu.

Ukiangalia Mathayo 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Chochote tunachokitafuta au tunachokihitaji katika maisha yetu tutakipata endapo tutamtafuta Mungu awe msingi katika maisha yetu ndipo tutakapoona Mungu anavyokuwa pamoja na sisi kama alivyokuwa na Joshua baada ya Musa mtumishi wake kufa.

Tumwombe Yesu Kristo awe pamoja nasi katika maisha yetu ili tufanye maamuzi sahihi ya kuutafuta ufalme wa Mungu. Pia Mungu ameahidi tukimtafuta yeye hayo yote tunayoyaangaikia atatuzidishia, katika jina la Yesu Kristo, Amen.
 
Amen,hivi ni wakati gani hasa tukimtafuta Mungu atatuzidishia hayo yote tunayoyafafuta?
[emoji843]Watu wengi wamekua wakimwamini Mungu na kuomba katika Yesu kristo lakini bado wanakabiliwa na matatizo je ni nini tatizo hapo?
[emoji843] Nini kinafanya watu wengi kuendelea kua masikini katika mfano Tanzania na Afrika ilihali watu wengi wanamwamini Mungu?Je ni kweli kwamba nchi kama China na Marekani wanaamini Mungu na Kristo ndio maana vitu vingi wamezidishiwa?
[emoji843] Je wakristo wa kawaida wanaweza vipi kumsikiliza Roho mtakatifu katika maisha yao ya kila siku na watajua vipi wanaemsikiliza ndiye?
Asante.
 
Dear Member,
Nashukuru kwa maswali. Yanayofuata ni majibu. Ubarikiwe unapoyasoma.

Hivi ni wakati gani hasa tukimtafuta Mungu atatuzidishia hayo yote tunayoyafafuta?
Wakati wote unafaa kumtafuta Mungu kwa sababu maisha yetu yote yako mikononi mwake na yeye ndio kimbilio letu. Sawa sawa na Luka 18:1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa.

Watu wengi wamekua wakimwamini Mungu na kuomba katika Yesu Kristo lakini bado wanakabiliwa na matatizo je ni nini tatizo hapo?

Mungu hawai wala hachelewi anajibu kwa wakati ambao ni sahihi. Kwahiyo wakati wa binadamu sio wakati wa Mungu pia wakati wa Mungu sio wakati wa binadamu, hata wakati wangu mimi sio sawa na wakati wako. Kila mtu ana nyakati na majira yake. Mungu anatujuwa sisi zaidi ya tunavyojijuwa.

Nini kinafanya watu wengi kuendelea kua masikini katika mfano Tanzania na Afrika ilihali watu wengi wanamwamini Mungu? Je ni kweli kwamba nchi kama China na Marekani wanaamini Mungu na Kristo ndio maana vitu vingi wamezidishiwa?

Kila nchi wanamwamini Mungu na bidii yanayoiweka kwa Mungu kwa kumuabudu na kumtukuza ndivyo Mungu anavyowakumbuka.
Kumbukumbu la Torati 7:9 Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu; 11 Basi zishike amri, na sheria, na hukumu ninazokuamuru leo, uzitende. 12 Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako; 13 naye atakupenda na kukubarikia na kukuongeza tena ataubarikia uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, maongeo ya ng'ombe zako, na wadogo wa kondoo zako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa. 14 Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mtu mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa mifugo.
Zaburi 1:1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. 2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. 3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Mathayo 4:4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
1 Samweli 1: 1 Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu 2 naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto. 3 Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea Bwana wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa Bwana, walikuwako huko.
Ayubu 1:6-22 Soma hii habari ya Ayubu uwone jinsi Mungu anavyoruhusu upitie changamoto/mapito mbalimbali kwenye maisha ili tu ajuwe kama bado anaweza kujivunia wewe mtoto wake kwa shetani.
Pia soma 1 Samweli 1:5 lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo.

Je wakristo wa kawaida wanaweza vipi kumsikiliza Roho mtakatifu katika maisha yao ya kila siku na watajua vipi wanaemsikiliza ndiye?
Mkristo akiokoka kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mokozi wa maisha yake ndipo anapopata NEEMA ya kumpokea Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 5: 32 Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio.
Yohana 14: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Yohana 4 :23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Matendo ya Mitume 5: 3 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? 4 Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. 5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.
Mathayo 10: 19 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. 20 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.

Mungu wetu mwema akulinde na kukufanikisha katika yote umwombayo, Amen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…