Godfrey Idew
New Member
- Nov 1, 2021
- 1
- 2
Suala la kuthamini utamaduni wetu katika nchi zetu za Afrika, mfano Tanzania limekuwa changamoto kubwa sana. Utamaduni wetu umeonekana kuwa taka, unaonekana kuwa ushamba na kuonekana kama mambo yaliyopitwa na wakati. Tumekuwa tukithamini sana tamaduni za kigeni, ilihali haziendani na sisi na mazingira yetu pia. Japo zipo zenye faida Ila nyingi zimekuwa zenye sifa mbaya na zisizo na maadili, mfano mitindo ya mavazi, vyakula visivyo na afya na tabia kama ushoga na usagaji.
Watanzania na Waafrika kwa ujumla tunapaswa kubadilika. Tunapaswa kupambana na kuhakikisha sisi tunaheshimika duniani kote. Hatuwezi kuheshimika kama sisi binafsi na utamaduni wetu tunajidharau na kujiona wa chini na tusio na maana. Nchi yetu ina tamaduni njema sana na zenye ubora wa hali ya juu, mfano nidhamu kwa kila mtu, kula vyakula vyenye afya, mavazi ya kimaadili, uchapakazi, ushirikiano na michezo ya ukakamavu. Tukizidumisha na kuzikuza zitakua na zitavutia wengi zaidi hata kutoka nje ya bara letu.
Waswahili wanasema "usipoziba ufa utajenga ukuta". Kwanini tusubiri ufa huu usababishe ukuta kuanguka ndipo tushughulike? Kwanini tusubiri utamaduni wetu ufe ndipo tushtuke toka usingizini? Kwanini tusichukue hatua mapema?
Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha inaleta ufufuo na kukuza utamaduni wetu ilianzisha Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikwa Tangazo la Serikali Namba 1 la Januari, 2016. Lakini pamoja na juhudi hizi bado tumeathiriwa sana na tamaduni za nje na kutokuthamini tamaduni zetu. Serikali yetu kwa kushirikiana na wananchi wake tunapaswa kuchukua hatua mapema kujikomboa kiutamaduni. Hii hapa Mikakati na njia mbalimbali ambayo inaweza kutumika kukomboa utamaduni wetu, kuukuza, kuudumisha na kuurithisha kwa vizazi vijavyo:
Kukuza ufahamu wa tamaduni za Kitanzania: Wengi wa Watanzania hasa watoto wamekuwa katika giza la kushindwa kuzitambua tamaduni halisi za kitanzania, tamaduni bora na zenye maadili, mfano uhusiano mwema na wengine na maadili mema katika jamii. Ili kuweza kukuza ufahamu, serikali na wadau wanapaswa kuandaa programu za elimu juu ya utamaduni wetu bora katika maeneo muhimu Kama shule, vyuo vikuu na jamii ili kuweza kusaidia kuongeza ufahamu kwa watoto na wananchi kwa ujumla kuhusu tamaduni za Kitanzania na umuhimu wake katika maendeleo binafsi, kwa familia, jamii na taifa kwa ujumla.
Kuzipa kipaumbele tamaduni zetu: Watanzania wengi wameathiriwa sana na utamaduni wa nje ya Africa hasa utamaduni wa nchi za ulaya na magharibi. Wanaziona kama ndiyo ustaarabu na usasa. Mtu anayevaa mavazi ya kimagharibi, lugha za kimagharibi au mtindo wa maisha ya kimagharibi jamii inamuona kama aliyestaarabika na mwenye elimu, lakini kiuhalisia si hivyo. Tunapaswa kuthamini cha nyumbani. Tunapaswa kuwa wazalendo wa utamaduni wetu. Wadau na serikali yetu inaweza kuboresha mazingira ya kazi na maisha ya wataalamu wa tamaduni ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi, kuwapa kipaumbele wote wanaofanya kazi zao kwa kuthamini utamaduni wetu. Pia, serikali inaweza kuokoa sehemu za kihistoria na maeneo muhimu ya utamaduni yanayohusiana na tamaduni zetu ili kudumisha utamaduni wetu kwa sasa na kwa kizazi kijacho.
Kuunda vituo na maeneo muhimu ya kuhifadhi utamaduni : Utamaduni wetu usipotunzwa vizuri unaweza kudumaa ama kufa kabisa. Ili tuutunze, yahitajika kuwa na vituo maalumu na maeneo maalumu ili kuhifadhi na kila mwananchi aweze kutembelea,kuona na kujifunza. Serikali au wadau wa maendeleo wanaweza kuanzisha vituo vya utamaduni katika maeneo mbalimbali ya Tanzania hususani mikoani, wilayani hata vijijini ili kuweza kuhamasisha uthamini wa tamaduni zetu. Vituo hivi ni kama vile makumbusho, maonyesho ya utamaduni, matamasha na mengineyo. Hii itasaidia kuwafanya wananchi kufurahia, kuimarisha utamaduni wa Kitanzania na kuvutia watalii pia.
Kuhamasisha ushiriki wa jamii: Ushiriki wa jamii yetu katika kukuza utamaduni wetu huthaminisha sana utamaduni. Jamii inaposhiriki kwa vitendo huongeza uelewa mkubwa, kupenda na husaidia kurithisha kwa wengine zaidi hasa kizazi kijacho. Ushiriki huu unaweza kuhusisha matukio ya kitamaduni, kama vile mashindano ya ngoma za asili, michezo matamasha na maonyesho ambapo wananchi wanaweza kujifunza na kuthamini tamaduni zao. Hii inaweza kufanywa kwa kutoa motisha na zawadi kwa washindi.
Kupitia sanaa: Nchi za Africa ikiwemo Tanzania tumejaaliwa vipaji vya kisanaa. Kama wasemavyo waswahili "mcheza kwao hutuzwa" basi inatupasa kuvipa thamani vya kwetu. Tukiwatumia wasanii wetu hawa vema tunaweza kuukuza na kuutangaza utamaduni wetu. Mfano, kwa kukuza sanaa za Kitanzania kama vile ngoma, muziki, filamu, na uchoraji na kutumika katika matamasha mbalimbali ndani na nje ya nchi inaweza kusaidia kukuza utamaduni wa Kitanzania na kusambaza ujumbe wa umuhimu wa tamaduni zetu.
Utamaduni unaanza kutengenezwa nyumbani katika ngazi ya familia ndipo unahamia ngazi ya jamii. Unaanza na baba na mama kuwafundisha watoto utamaduni mwema kama vile nidhamu, nafasi ya mwanamke na mwanaume, mavazi bora, mazoezi na kujali afya. Tunatakiwa kubadilika na kuthamini vyetu. Hata wageni wanapenda kuona kitu kipya na ndiyo kivutio cha watalii. Hivyo, hatua hizi zinaweza kusaidia, kubadili mitazaml na kuwezesha Watanzania kukua, kuthamini na kuimarika kitamaduni.

Attachments
Upvote
2