Hakuna barabara isiyo na kona

Hakuna barabara isiyo na kona

josam

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Posts
2,252
Reaction score
1,041
Mara zote hakuna barabara isiyo na kona hata iwe ya lami.

Mimi ni sihitaji kujitambulisha ni mwanachama wa chama gani ila ukifuatilia michango yangu humu jamvini utajua nini msimamo wangu na hautabadirika kwa sababu najua nini faida ya kuwa na vyama vyenye nguvu sawa katika taifa. Mkiwa sawa kila anaye pata nafasi anawajibika ipasavyo. Hata kinachifanyika leo ni kwa vile tu kudra imetokea, watu walielewa somo na mchango wa magwiji wa Siasa.

Swali,

Mwananchi gani asiye chukia rushwa, uongozi mbovu usio tumia vizuri rasilimali za taifa kwa maendeleo ya taifa na mengine yenye mwelekeo huo???

Binafsi nilijaribu kuanzisha biashara hapa Tanzania ila mazingira hayakuwa rafiki, na katika footer za nyaraka za kampuni yetu tuliandika neno 'rushwa ni adui wa maendeleo'. Na nilishauri wenzangu sitaki kusikia kampuni imetoa rushwa! Matokeo yake, tupo palepale hatunyanyuki. Kila tangazo la kazi ikitokea anaye toa fungu kubwa ndiye anayepewa kazi, imefika mahali siyo 10% ni karibu 30% ya gharama ya kazi. Rushwa imekuwa siyo katika kazi tu hadi kwenye ofisi. Tena hakuna hata kificho, huna anaye kufahamu, huna rushwa hupati huduma kwa usawa au hupati kabisa.

Ni kama wafanya biashara walio wengi mfano kariakoo, mtu yupo jasiri kabisa anakwambia bei ya bidhaa hii ni kiasi hiki na kama na VAT ni kiasi hiki unalipa ipi? Unajiuliza jiji hili ndiyo makao makuu yetu, Ikulu ipo hapa, ofisi zote zinazo fuatilia mambo ya fedha, TRA, PCCB, nk wote wamejazana mji huu, huyu jamaa anajiamini nini kiasi hiki. Unabaki mdomo wazi, ukipima kwamba je, VAT hii ninayo ambiwa nilipie inatumikaje? Unajua ni kununulia mashangingi, kulipana posho na marupurupu kibao, kikao kinafanyika gorofa ya tatu ila anayehudhuria hata kama ofisi yake ipo gorofa ya nne sitting allowance anadaka kama kawa, chaki hakuna, vidonge sipati, umeme sipati bali nachafuliwa hata na hewa niliyojaliwa na Mwenyezi, Maji sina, mipango miji kizungumkuti, na mengine mengi, unaona bora usilipe hiyo VAT 'maana ni kwa manufaa yao' walau nawe usevu hiyo!

Nani anapenda mambo hayo yaendelee? Wewe?

Kuna watu waliishi kwa mishahara tu na kuna watu waliishi kwa posho na marupurupu bila kugusa mishara yao. Pia kuna ambao wao ndiyo kika kitu, wanatunga sheria (wenzao ndiyo wasimamizi wa sheria hizo), hawataki waguswe na sheria hizo. Hao Ndiyo waliobakia wanaishi kwa mapato ya marupurupu na posho, mikopo nafuu (kwa mikopo usawa huu sina hakika kama inatoka... Kwi..kwi...), hawa ni wanaoitwa waheshimiwa na wazee wa suti kwenye ofisi zao. Hawa ndiyo waliosoma ama kubahatika kuwa mheshimiwa hata kama shule hawana.

Uchumi unaweza kutetereka hivyo kujikwaa. Kujikwaa huku kunaweza kuturambisha ardhi ila nina imani tukisimama tutapiga hatua vizuri.

Kwa mara nyingine tena, hakuna barabara isiyo pita katika milima na mabonde.

Kama viongozi wetu wawe tuliowachagua wenyewe au kuchaguliwa ama vyovyote ujuavyo, iwapo WANAJUA TUNAKO ELEKEA BASI TUTAFIKA. Ila kama hawajui tunako kwenda njia yoyote itatupeleka japo tunaweza tusifike!

Mungu akubariki kwa kusoma ujumbe huu!
 
Back
Top Bottom