mwibamwiba
Senior Member
- May 22, 2015
- 150
- 38
Duniani kote hakuna biashara yenye faida kubwa kama hii, hakuna biashara yoyote ulimwenguni unayoweza kuifananisha nayo si ya mafuta wala almasi wala silaha za kivita na hakuna biashara nyepesi katika ufanyikaji wake kama hii, wao wanacheza na code tu basi huku wanacheza game na kunywa juice, nayo ni wenye makampuni ya simu na uuzaji wa vocha. Ila swali langu ni nani kashajiuliza ni nani hasa anaemiliki biashara hii, Je, ni nchi au kundi la watu au CIA, maana kama taifa lolote ulimwenguni lingetaka kuwekeza na kupata faida lingeanzisha biashara hii, Je kuna ugumu wowote kuianzisha maana vocha za simu zinanunuliwa kwa maelfu kote ulimwenguni na hapo ndio ninapata wasiwasi na takwimu za hisa ni kweli simu inazidiwa na viwanda vya cement.
Naomba ufafanuzi
Naomba ufafanuzi