The_Cipher_TZ
Member
- Jul 4, 2026
- 11
- 21
UKWELI MCHUNGU
Hakuna Bilionea wa Kazi Halali, Formula ya Siri ya Utajiri Ambao Hamuambiwi popote zaidi yangu.
Wakuu, leo nimekuja kuwapa taalifa ya moto, na najua kabisa mtaukataa huu ukweli kwa sababu unauma, mtatokwa na povu la kijani na kuanza kuleta habari za maadili na vitabu vya dini hapa.
Lakini mkimaliza kulia na kupiga kelele, wekeni chini mihemko yenu, mkae chini msome hiki nilichokiandika hapa kwa akili ya baridi na mtajua kwanini mnaendelea kusugua benchi huku wenzenu tunatoboa.
Dunia hii ina sheria zake zilizowekwa makusudi kabisa na mfumo ili wachache wafurahi na wengi waumie maisha yao yote. Sheria hizi za kijamii na kisheria zimeundwa ili zikuweke wewe kwenye mstari kama kondoo, uendelee kuwa mtumwa wa tabaka la juu, ulipe kodi, uwaajiri watoto wao, na ufe ukiwa maskini uliyejaa sifa za "huyu alikuwa mtu mwema sana.
Ukitaka kuwa tajiri wa kweli kwenye ulimwengu huu, lazima uwe na uthubutu wa kichaa wa kuvunja sheria za mfumo zilizowekwa mbele yako.
Acheni kudanganyana mchana kweupe hapa jukwaani, hakuna mtu anayetajirika na kuwa bilionea kwa kufuata njia zilizonyooka mia kwa mia.
Kazi halali, ajira za serikalini au binafsi, biashara za kawaida za kutoa risiti kila sekunde, na kilimo cha jembe la mkono au cha kufuata miongozo ya maafisa ugani, vitu hivyo vyote vitakupa tu hela ya kula, kulipa kodi ya pango, kujenga kanyumba ka kawaida ka familia, na kununua kagari ka kawaida ka kutembelea ili usinyeshewe na mvua.
Basi, maisha yanaishia hapo, Ukitaka kumiliki bilioni moja au zaidi kwenye akaunti yako ukiwa bado una nguvu, ukiwa kwenye huu umri wa ujana wa miaka 25, 26 hadi 40, sahau kabisa habari ya kuwa kijana mwema, mpole na anayeogopa kila kivuli.
Wema haujawahi kuleta utajiri wa kutisha mahali popote duniani, na ukitaka utajiri wa kiwango cha juu, lazima uvunje sheria na ucheze nje ya mstari uliolazwa.
Huu ulimwengu mnauona wa amani mkiwa mmetulia mbele ya vioo vya simu zenu ni uongo, maisha ya juu ni vita ya kiintelijensia, ni mapambano ya nguvu na mbinu chafu ambazo hazifundishwi kwenye darasa lolote lile.
Kwenye hii miaka yenu ya ujana, unadhani utafanya kazi gani halali, ya jasho la halali kabisa, ikuingizie mabilioni ndani ya muda mfupi bila kuwepo kwa mbinu chafu na za kimkakati nyuma yake?
Lazima ujue kucheza na akili za watu, lazima ujue wapi pa kupiga gap na wapi pa kuingiza utapeli wa kiwango cha juu, kwa sababu kwenye ulimwengu wa biashara kubwa, usipowapiga gap wenzako na kuwaacha chini, wao ndio wanaokupiga wewe na kukuacha ukilia.
Waliofanikiwa na wanaomiliki miundombinu mikubwa wanajua jinsi ya kupita katikati ya sheria bila kukamatwa, wanajua jinsi ya kucheza na mifumo na mamlaka mpaka mfumo wenyewe uwaogope au uwatumikie.
Hakuna anayetoboa kileleni akiwa msafi kama theluji, kila utajiri mkubwa unaoona hapa mjini una siri nzito na ya kutisha nyuma yake, iwe ni nguvu za giza zinazotumika kudhulumu nyota za wengine, siasa chafu za kukataza wengine wasishindane na wewe, ukwepaji wa kodi wa kiwango cha juu cha kisheria, au dili za pembeni na makolokocho ya kila namna yanayofanyika usiku wa manane wakati ninyi mkiwa mme lala mkiota kwenda mbinguni.
Amkeni ninyi vijana, kwani maadili na sheria hizi mnazozitukuza zinasimamiwa na kutengenezwa na maskini wanaotaka kujifariji.
Matajiri wakubwa ndio wanaofadhili sheria na maadili mnayohubiriwa usiku na mchana ili ninyi mbaki kuwa raia wema mnaotii na wanyenyekevu, huku wao wakiendelea kuvuna rasilimali zote na kuwaacha ninyi mkigombania makombo.
Unakaa hapo unajisifia kwa majivuno kabisa kwamba unafanya biashara halali na hutaki dhambi, huku mtoto wako anakosa ada ya shule nzuri, wazazi wako wanaishi maisha ya shida kijijini, na mkeo anapanda bodaboda kwenye mvua ya mawe, huo sio wema wala ucha ungu, huo ni uoga uliopitiliza uliovishwa koti la uaminifu.
Kama ndoto yako ni kumiliki akaunti yenye tarakimu tisa na kuendesha mashine za kifahari hapa mjini, anza kubadilisha mtazamo wako kuanzia sekunde hii, acha uoga wa kijinga kwani maisha hayajawahi kuwa ya haki na hayatakuja kuwa ya haki kamwe.
Kama unataka kuwa simba kwenye msitu huu wa kizazi kipya, lazima ukubali kuwinda, kukabiliana na hatari, na hata kumwaga damu kwa kunyonga sheria, lakini ukichagua kubaki kuwa kondoo mpole, sahau habari ya mabilioni na ukubali kuliwa ukweli ndio huo.
Mada ipo mezani, leteni mapovu yenu.
Tafuta hela miaka 30 na huna hata kiwanja sio sifa.
Mwisho.