Hakuna dhambi kubwa na isiyo sameheka kama zambi ya kumwaga damu ya binadamu

Hakuna dhambi kubwa na isiyo sameheka kama zambi ya kumwaga damu ya binadamu

joseph2

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
458
Reaction score
1,032
Habari ndungu zangu wana JamiiForums.

Ni matumaini yangu kuwa wana JamiiForums na watanzania wote popote mlipo mtakuwa mnaomboleza kifo cha ndugu yetu Ally kibao,

Taifa letu limefika mahali pabaya sana na halikufika hapa kwa bahati mbaya au kwa mda mfupi. Taifa letu limefika hapa sio kwa sababu ya watawala wabaya au waovu.

Taifa letu limefika hapa kwa sababu ya ukimya Watazania wema. Watu wema tumekaa kimya kwa muda mrefu, eidha kwa kudhani kukaa kimya ndio salama yetu au kukaa kimya ndio njia ya kutuepusha na watu wabaya.

Njia zote hizo sio tu hazisaidie Bali pia njia hizo zinawafanya watu wema kuwa wabaya kuliko hata wanao tenda uovu kama huo alio tendewa ndugu yetu Ally kibao.

Watanzania wote tulio umizwa na kitendo hiko kiovu kabisa kuliko vyote alicho tendewa ndugu yetu Ally kibao, Kiwe kengere ya kuamusha watu wote wema kusimama na kusema sasa imetosha. Tuchaguwe moja. Waovu watuuwe wote ili wabaki peke yao na Tanzania ijulikane kama taifa la waovu . Au watu wema wote tusimame pomoja tuwadhibiti waovu kwa kutumia sheria za haki na nguvuv ya uma ya kukataa uovu.

Kama binadam anapo fikia hatuwa ya kuuwa binadamu mwezake kwa sababu ya mali au cheo huyo sio binadamu tena . Anaposwa kuondolewa kwenye jamii . Sasa kama Tanzania imefika mahali watu walio jitowa ubinadamu na kuwa wauwaji wanaachiwa huru na kuendelea kuishi kama binadamu basi taifa letu lipo katika hali mbaya sana.

Ni hivi katika jamii yoyote mtu aliye mwaga damu ya binadamu mwingine. Hasitahili kuishi tena kama binadamu. Ebu tufikiri kwa pamoja. Pesa ni karatasi ambazo binadamu alibuni kwaajiri ya kusaidia binadamu wezake kubadilisha vitu na huduma kiulahisi. Sasa ina kuwaje uuwe mtu ili update pesa wakati mtu ndiye katowa wazo la kutengeneza pesa? Yaani mtu anaye uwa mwanadamu mwezake ni sawa mpumbavu anaye choma gari lake mpya ili akauze chuma chakavu. Mtu mwenye fikra hizo akili zake ziko chini sana kuliko hata mnyama mjinga kama nguruwe. Kwani hata nguruwe pamoja na kula uchafu wa kila aina lakini hawezi kula nguruwe mwezake .

Tena ni nadira sana mnyama yoyote kuuwa mnyama mwezake wa aina yake. Sasa inakuwaje binadam unauwa binadamu mwezako kwaajiri ya kutaka mali au cheo? . Hivi kweli unawezaje kufurahia mali au cheo huku ukiwa unajuwa mali au cheo chako kimepatikana kwasababu ya damu ya binadamu mwezako? Mimi Sina dini ila na amini kusudi la uhai wa binadamu wote ni kutatuwa matatizo ya binadamu wezeke hapa duniani Ili Dunia iwe pahala pema pa binadamu kuishi kwa Amani na furaha.

Ndio maana kila jamii inakuwa na taratibu za kupata viongozi wa kuongoza juhudi hizo za kufanya Dunia kuwa salama kwa binadamu. Ukiona mtu analazimisha kuongoza wengine bila ridhaa ya watu anao taka kuwaongoza huyo naye ni mpumbavu wa kiwango cha chini kabisa. Kusudi la kuongoza watu ni kutaka kusaidia watu kwa kuunganisha mawazo yao katika kutafuta suluhisho la matatizo yao. Sasa inakuwaje mtu unaamuwa kutumia nguvu ili uwe kiongozi ?

Na yasema haya kwa sababu naamini huu uovu wa kuteka watu na kuwauwa unao endelea Tanzania unauhusiano wa moja kwa moja na watu wanao Andaa njia za kupata madaraka ya kiutawala kwenye chaguzi zijazo hivi karibuni. Binadamu mwenye akili timamu hawezi kuuwa binadamu mwezake kwaajiri ya madaraka au mali.

Watanzania tujitafakari turudi kwenye ubinadamu. Tunako elekea sio kuzuri. Kama tumeanza kuona vyeo na mali ni bora kuliko uhai wa binadamu basi tujihesabu kuwa tunatengeneza taifa la wapumbavu. Mali na vyeo ni ubunifu wa binadamu Sasa iweje wazo la binadamu liwe na thamani kuliko binadamu mwenyewe.

Naomba niishie hapa. Mwisho Mungu uilaze mahali pema peponi roho ya ndugu yetu Ally kibao. Pia na towa rai kwa Watanzania siku yoyote mkiona mtu anakamatwa lazima mjitokeze kuwauliza hao wanao mkamata mtu wanampereka wapi . Ikibidi msindikizeni mpaka wanako mpereka. Kama abiria kwenye bus alilo kuwemo Ally kibao wangechukuwa hatuwa za kuwauliza hao majambazi walio muuwa Ally kibao huenda hali ingekuwa tafauti..

PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ally Mohamed Kibao, kiongozi wa chadema auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
 
Back
Top Bottom