Hakuna elimu Bure, elimu ni gharama sana, wazazi tuwajibike

Hakuna elimu Bure, elimu ni gharama sana, wazazi tuwajibike

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Elimu ni Pana sana haiwezi kutolewa Bure, serikali haina huo uwezo.
Kuna wazazi wamebweteka tu kuwajibika Kwa watoto wakijodai ati serikali inatoa elimu Bure.
Viongozi wa serikali hawasomeshi kwenye hizi shule zenu za vumbi, kidumi na mfagio watoto wao wapo international school wanalipa ada Kwa dollar 💵💰

Elimu inajumuisha ubunifu, mazingira, majaribio, maabara, kazi za mikono, tehama. Shule za public hazina viwanja, maktaba, maabara, computer na mashamba. Watoto wanakaa darasani kama mifugo ya Masai zizini
Watoto hawapati chakula wanashinda shule na njaa hivi kweli mtoto atasoma aelewe akiwa na njaa kutwa nzima. Walimuuza hawatoshi, madawati hamna, madarasa hamna n.k

Elimu sio kuwa sare na madaftari tu. Watanganyika msitumike na wasiasa kuambiwa ati elimu Bure ni vizuri kuchangia Kwa kulipia ada ili madarasa yajenge, chakula n.k. Wanasiasa hata diwani hawapo kwenye shule za St kayumba, kidumu na mfagio, vumbi n.k
 
Back
Top Bottom