Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 276
- 460
Kila hatua unayopiga kwenye maisha ipime kwa kuangalia ulikotoka. jiulize jana na juzi nilikuwa wapi leo niko wapi, majibu yake yatakupa taswira kama unapiga hatua au unarudi nyuma.
Wapo wengi ambao hupima mafanikio yao katika nyanja moja tu ya maisha "hali ya kiuchumi" pasipo kuangalia mafanikio katika nyanja zingine za maisha.
Utakuwa umefanikiwa kiuchumi lakini huwezi kuishi kwa amani kama mali zako umezipata kwa unyang'anyi na ushirikina, maisha yako yatajaa majuto moyoni na utaonekana mwenye furaha usoni.
Hata hivyo hakuna furaha ya kweli anayoipata masikini aliye timamu kiakili duniani, umasikini ni nyumba ya huzuni, kero na kuonewa hivyo ili kuwa na furaha ya kweli unahitaji pia kuimarika kiuchumi.
Mbali na hayo mafanikio yako yatapimwa vema iwapo una afya bora, kwani ukipata vyote na ukose uimara wa kiafya kamwe huwezi kufurahia mafanikio yako yoyote yale.
Je wanaokuzunguka wanakufurahia wakikuona? Wanakuchukia tu au kuna sababu yenye doa unayo kwenye mioyo yao?
Ukifanikiwa kiuchumi jiulize umefika wapi katika mafanikio ya kijamii, kiimani na kadhalika.
Fanya yote lakini usisahau kuwa "bila Mungu hutoboi" Tafakari.
[emoji2398]Peter Mwaihola