Hii habari nafikiri ni ukweli kwamba makaratasi yalikuwepo ndani ya malori.
Mzigo umefika Tunduma, umekaguliwa na TRA, kawaida polisi hawahusiki kwenye mambo ya mapato ila tu kama kuna fujo au uvunjifu wa sheria.
Sasa aliyewaita polisi ni nani kwa ajili ya nini?
Kwa nini IGP aliongelee na kusema polisi walikagua lori kuangalia kama kuna karatasi za Kura.
Ni nani aliyewafanya polisi kukagua kwa ajili ya kutafuta kura.
Je ni kweli mpakani kuna mizigo inawafanya polisi wa vikosi vyote waende kama hakuna fujo?
Je Taarifa iliyopelekwa na Polisi na TRA ilikuwa ikisema nini?
Na kama tuhuma zilikuwa ni karatasi za kupiga kura waandishi wahabari waliitwa?
Hii habari inabeba ukweli kwa asilimia za kutosha, uwezekano wa kwamba polisi walikwenda kuzilinda ni mkubwa, kazi tuliyonayo ni kutafuta polisi waliokwenda kulinda zile nyaraka wako wazalendo watasema tu.
IGP kumbuka EPA, mlikataa hata Raisi wako alitoa lugha za kashfa kiko wapi leo?