SoC01 Hakuna haja ya kudai Demokrasia

SoC01 Hakuna haja ya kudai Demokrasia

Stories of Change - 2021 Competition

Gwanxoo

Member
Joined
Jan 24, 2021
Posts
9
Reaction score
3
Jamani ili demokrasia iwepo lazima udikteta uwepo maana kama kwenye kuna demokrasia sasa tunakuwa tunadai nini?

Udikteta au maendeleo. Na ubaya wa waafrika tunadai demokrasia badala ya kudai maendeleo maana Mimi naamini maendeleo na mabadiliko ya kimaisha yanamfanya mtu kusahau udikteta...Rwanda...

Sasa Basi udikteka ndio huleta demokrasia na kitu kizuri cha kujifunza ni kwamba udikteta unaweza ukanunua demokrasia lakini demokrasia haiwezi kununua udikteta na ndio maana mtu akidai sana demokrasia kuna wakati akishindwa kukubaliana na udikteta anaishia maisha magumu, kuangaika, kuchoka lakini mbaya zaidi ni kama hoja zake hazisikilizwi jambo ambalo hutia hasira.

Na kudai demokrasia ni sawa na mtu maskini anaishauri jamii mbele ya mwenye pesa katika jambo linalohitaji pesa hakika abadani hawezi sikilizwa hata siku moja.

Sasa basi kwa sisi waafrika tubadilishe mfumo badala ya kudai demokrasia tudai maendeleo maana hata kama mtu akiwa dikteta lakini anafanya maendeleo basi inatosha maadamu yeye ni mwanadamu atakufa basi siku akifa maisha yaendelee ila tunahitaji maendeleo ya taifa yanayotoa fursa za maendeleo ya mtu mmoja mmoja

Tuachane na kudai demokrasia hebu tuangalie mambo ya msingi je yanatimizwa mambo mengine yaendelee. Lasivyo tutaongea na tuta tweet lakini wapi maana hoja ya masikini hazisikilizwi, na nikwambie tu kila nchi duniani ina udikteta ndani ambao wenye akili tu ndio wanaoelewa.

Hahahaha
Hii ni kuongeza idadi ya maneno
 
Upvote 2
Kwa dhana hii naona kama hutofautishi kati ya "kukua kwa uchumi na Maendeleo" uchumi unaweza kukua lakini maendeleo hayamwitaji dikteta hata siku moja, iwapo katika Taifa mambo yanaendeshwa kidikteta maana yake hata huduma hazitatolewa kwa usawa.
 
Sidhani sana lakini ishu kubwa ni mtu mwenyewe anaekalia kiti kama hana nia au shauku ya maendeleo nakuhakikishia atafanya vibaya hata kama demokrasia ipo au haipo...mfano mzuri Libya au China miaka ile viongozi wao walionekana ma dikteta lakini walifanya mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo ndani ya taifa...so ni vile mtu alivyo ndio maana kuna umuhimu sana wa kiongozi uwe na mataminio chanya wewe binafsi yani hata iweje uyafanye miaka itaisha utatoka kuliko kuwekwa tu kama gari bovu litakalokuja lifanywe...
 
Suala la Uongozi si suala la Mtu alivyo, suala la mfumo unaomweka madarakani yeye, mfumo ndio unaoamua nini kinapaswa kufanyika, iwapo kiongozi anakuwa na yake maana yake analazimisha mfumo umuondoe madarakani. Dikteta anaweza kukuza uchumi ila haweza kuleta maendeleo kwasababu vitu siyo watu, hata huduma katika Taifa haziwezi kuwa katika focus ya maisha ya watu, China mpaka leo watu bado wananyongwa na wakati mwingine without single opportunity of freedom of expression. Kinachohitajika siyo personal thought kwenye uongozi kinachotakiwa ni nchi kuendeshwa kitaasisi.
 
Okay vizuri lakini inatakiwa tubadilike kwa maana maendeleo ni personal na uchumi ni general sasa nakuuliza swali kipi kinamzaa mwenzake kati ya uchumi na maendeleo?
 
Back
Top Bottom