Hakuna haja ya kuogopa kufa kama hukujua ungezaliwa

Hakuna haja ya kuogopa kufa kama hukujua ungezaliwa

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039

Dini zimekuwa zikitumia kifo kama dhana ya kutisha toka na ujinga na ujanja ujanja wa kutaka kuwatisha ili kuwatawala na kuwaibia waumini. Mara utaingia motoni, mara peponi. Nani amewahi kwenda kule? Wengine huenda mbali na kuelezea ilivyo pepo au motoni. Yote uongo mtupu. Ni ngano za kutishana ili kunyonyana.​

Kama ulivyokuwa hujijui ulipozaliwa, ndivyo itakavyokuwa utakapokufa.​

Utarudi kwenye hali uliyokuwa nayo.​

Hivyo, hakuna haja ya kutishana au kutishwa na ngano za kijinga za kubuni.​

Kifo ni sawa na. hali nyingine za kimaumbile.​

Ukiwa hai, jua utakufa.​

Ukiwa kijana, jua utazeeka.​

Ukiwa mzima, jua utaugua.​

Ukiwa na nguvu, jua utakuwa dhaifu.​

Ukiwa na furaha, ujue utasikitika.​

Ukiwa mgonjwa jua utakuwa au ullikuwa mzima.​

Ukikosa, ujue utapata na ukipata, ujue utakosa.​

Huwezi kupata au kukosa yote.​

Huwezi kujua au kutojua yote.​

Ukipenda, jua utachukia.​

Ukisifiwa, jua utalaumiwa.​

Hii ndiyo asili ya kila kitu.​

Kuna uwili hata zaidi.​

Bila giza, hakuna mwanga.​

Bila ubaya, hakuna uzuri.​

Bila utepetevu, hakuna ujabali.​

bila njaa, hakuna shibe.​

Bila machozi, hakuna kicheko.​

Bila maumivu, hakuna nafuu.​

Bila umaskini, hakuna utajiri.​

Je tajiri hamtegemei maskini?​

Je. maskini anamtegemea nani?​

Ke na Me hazitegemeani?​

Bila hivyo, nani angekuwa hapa?​

Hiyo ndiyo busara ya leo.​

Sasa mbona tukiuguza wagonjwa wetu siku wanakata roho baadhi yao huhangaika mno na macho yanawatoka mkuu??tena wengine haja ndogo na kubwa huwatoka kabisa..je kwa uelewa wako hii ni dalili nzuri kweli?? Unaenda sehemu yenye amani au furaha ila ni kwa taabu na mateso hivi dahh..haya bana
 
Ukielewa kuwa kinyume cha kupata ni kukosa na kuishi ni kufa na mwanzo ni mwisho, hutaogopa wala kujihangaisha na jambo ambalo huwezi kulizuia mwanangu.
 
Sasa mbona tukiuguza wagonjwa wetu siku wanakata roho baadhi yao huhangaika mno na macho yanawatoka mkuu??tena wengine haja ndogo na kubwa huwatoka kabisa..je kwa uelewa wako hii ni dalili nzuri kweli?? Unaenda sehemu yenye amani au furaha ila ni kwa taabu na mateso hivi dahh..haya bana
Hata kwenye "Climax kila mmoja Anareact kivyake..Na hakuna maumivu pale
 
Sasa mbona tukiuguza wagonjwa wetu siku wanakata roho baadhi yao huhangaika mno na macho yanawatoka mkuu??tena wengine haja ndogo na kubwa huwatoka kabisa..je kwa uelewa wako hii ni dalili nzuri kweli?? Unaenda sehemu yenye amani au furaha ila ni kwa taabu na mateso hivi dahh..haya bana
Si binadamu tu hata wanyama wanapitia hali hiyo ambayo imebase katika sayansi ya asili tofauti na hizo imani za kipuuzi za kidini.

Mtu anapoaga dunia kwa kifo cha asili ambacho hakiusishi ugafla kama ajali, lazima kupitia bugudha kadhaa kulingana/aina ya kitu kinachompelekea kufa, ikiwa kwa kujiua lazima ateseke, ikiwa kwa magonjwa vile vile lazima apitie process za utu wake kuuacha mwili kwa kipindi kifupi cha kupata picha za kumbukumbu alizopitia tangu mtoto mpaka alipo hapo ndiomaana baadhi ya watu hupiga kelele baada ya kuwaona wapendwa wake ambao alispend nao kipindi cha uzima, pia kuwaona baadhi ya watu ambao walishakufa lkn anapata kumbukumbu fupi alizospend akiwa nao.

Pia kuna kupata kumbukumbu za matukio makubwa aliyoyatenda au kuwatendea wengine iwe mabaya au mazuri, kifo chake kinakuwa cha utulivu kama atapitia kipindi cha kumbukumbu nzuri ambazo alispend maisha katika mambo mema, na hapo utaona mtu anakufa akiwa na faraja mpaka usoni na utulivu mkubwa, pia kwa baadhi hupitia majuto na bugudha kadhaa anapokufa sababu ya kupata kumbukumbu mbaya ya matendo aliyowatendea wengine, na hili huwatokea hasa ambao hawakumaliza vizuri maisha yao kwa kusolve matatizo/changamoto baina yao na waliowatendea iwe kwa kusameheana au kutubu makosa kwa mtendewa na kujisamehe,

Iko hivi kila mtu anapokufa kifo cha asili(si cha ghafla kama ajali) lazima apitie hiyo process wanayoita wataalamu "DEATH EXPERIENCE" inayohusu baadhi ya hekahekaza kimwili na akili kwa kupata kumbukumbu za matukio kipindi cha uhai wake pia kufutika kwa kumbukumbu zake zote huku likija suala zito ambalo wengi wamepotoshwa na dini ndizo zimelifanya kama siraha yao ya kudanganya jamii kua mtu anapokufa basi kuna mahala pa adhabu ya moto anakwenda au kuna mbingu anaenda jambo ambalo si kweli

Kufa ni mwisho wa maisha ya kiumbe duniani lakini ndio mwanzo wa muongozo wa maisha mapya ya Energy yako(Nafsi) yako ambayo ktk sekunde kadhaa unapokufa nafsi yako ndio huona hayo matukio ya maisha yako na huona kila jambo kwa wakati huo katika uhalisia wa maisha ya Nafsi na si mwili, yaani unapokua ktk process za kifo macho yako ya ndani ambaye ndiye nafsi(UTU) yanafunguka na kupata picha ya matendo yako iwe ya hovyo na mazuri si ajabu ukipiga kelele maana matukio hayo yanaweza kuambatana na kuona baadhi ya viumbe ambao ndie mizimu ambayo hubeba taswira za nduguzo waliokufa au ambao bado wangali hai.

Kinachofuata baada ya hapo ni kufutika kwa kila kitu, yaani kifo cha mwili ambapo akili hupotea na kufutika, inabaki nafsi ambayo watu wa dunia hawaoni, hapo ndipo unaingia katika maisha ambayo dini zimeyapotosha, huko kuna mambo yake pia,

Naishia hapa nisije wachanganya wengi, lakini niwakumbushe walio wengi ni kwamba maarifa ni jambo la maana sana, unapokosa maarifa unakuwa sawa na askari aliyekosa siraha vitani, hivyo kila adui anaweza kukupelekesha atakavyo, ni sawa na maisha ya waafrika baada ya kukosa maarifa ya maisha na asili wamebaki kupelekwapelekwa na hizo dini zinazowapotosha kila jambo na kuwatisha.

Kama kuna kuzaliwa basi kuna kufa na kuna kuzaliwa katika maisha yako ya wewe mtu wa ndani ambako ndiko nafsini kuna mambo yanaendelea.

Fanya mambo mema kwa wenzio, jitendee mema na uwatendee wengine mema, uone kama mwisho wako hautokuwa mzuri, tofauti na hizo dini zinazowajaza hofu,

Moto haupo, jehanamu haipo wala kuzimu haipo bali kuna ulimwengu ambao nafsi yako ndio inaishi na ndiko huko huko ukifa ktk mwili nafsi yako itabaki huko kuendelea na michakato ya kihaki na hukumu kulingana na matendo yako uliyofanya duniani narudia tena hakuna moto wala jehanamu ya moto bali upo ulimwengu ambao hata hivi sasa nafsi yako ipo huko na hata wewe ushawai kuingia ukiwa na utambuzi wa akili yako ya mwili au bila utambuzi wako (usingizi) hivyo basi si jambo la kuogopa.
 
Sasa mbona tukiuguza wagonjwa wetu siku wanakata roho baadhi yao huhangaika mno na macho yanawatoka mkuu??tena wengine haja ndogo na kubwa huwatoka kabisa..je kwa uelewa wako hii ni dalili nzuri kweli?? Unaenda sehemu yenye amani au furaha ila ni kwa taabu na mateso hivi dahh..haya bana
Hakuna maumivu wakati wa kukata roho,bali mwenye anakata roho akiwa na akili timamu huangaika kwa hofu ya kuogopa kufa ama kuanza kupoteza pumzi. Hii hauwezi ukaikuta kwa yeyote anae kufa kwa amani ama anaekufa akiwa usingizini mkuu.
 
Sijasoma ulichoandika ila naamini umeandika ujinga..
Kama unaona ujinga kwanini unakoment? hili suala la kutusi mada za watu bila research wala mchango wowote ni utoto wa hali ya juu, nina imani mtu mpaka anaandika na kuweka humu hajakurupuka bali kaandaa mambo ambayo kayafuatilia, sasa wewe ambaye ndie mjinga unawezaje kuhitimisha mada ambayo hujaisoma wala kuelewa zaidi ya kukoment kwa negative review kama hivyo?.

Waafrika tukiacha roho mbaya, chuki na uvivu wa kusoma mambo mapya tutafika mbali.
 
Dini zimekuwa zikitumia kifo kama dhana ya kutisha toka na ujinga na ujanja ujanja wa kutaka kuwatisha ili kuwatawala na kuwaibia waumini. Mara utaingia motoni, mara peponi. Nani amewahi kwenda kule? Wengine huenda mbali na kuelezea ilivyo pepo au motoni. Yote uongo mtupu. Ni ngano za kutishana ili kunyonyana.​

Kama ulivyokuwa hujijui ulipozaliwa, ndivyo itakavyokuwa utakapokufa.​

Utarudi kwenye hali uliyokuwa nayo.​

Hivyo, hakuna haja ya kutishana au kutishwa na ngano za kijinga za kubuni.​

Kifo ni sawa na. hali nyingine za kimaumbile.​

Ukiwa hai, jua utakufa.​

Ukiwa kijana, jua utazeeka.​

Ukiwa mzima, jua utaugua.​

Ukiwa na nguvu, jua utakuwa dhaifu.​

Ukiwa na furaha, ujue utasikitika.​

Ukiwa mgonjwa jua utakuwa au ullikuwa mzima.​

Ukikosa, ujue utapata na ukipata, ujue utakosa.​

Huwezi kupata au kukosa yote.​

Huwezi kujua au kutojua yote.​

Ukipenda, jua utachukia.​

Ukisifiwa, jua utalaumiwa.​

Hii ndiyo asili ya kila kitu.​

Kuna uwili hata zaidi.​

Bila giza, hakuna mwanga.​

Bila ubaya, hakuna uzuri.​

Bila utepetevu, hakuna ujabali.​

bila njaa, hakuna shibe.​

Bila machozi, hakuna kicheko.​

Bila maumivu, hakuna nafuu.​

Bila umaskini, hakuna utajiri.​

Je tajiri hamtegemei maskini?​

Je. maskini anamtegemea nani?​

Ke na Me hazitegemeani?​

Bila hivyo, nani angekuwa hapa?​

Hiyo ndiyo busara ya leo.​

Ume bold ili kuwatisha moderators?

Utaogopaje kifo wakati tulizaliwa ili tufe?
 
Tena watu kama nyie mkiona mtu anakufa mnapata wenge mpaka mnapiga Nduru
Naamini Mungu yupo sababu kuna vitu ni zaidi ya ufaham wetu
 
Sasa mbona tukiuguza wagonjwa wetu siku wanakata roho baadhi yao huhangaika mno na macho yanawatoka mkuu??tena wengine haja ndogo na kubwa huwatoka kabisa..je kwa uelewa wako hii ni dalili nzuri kweli?? Unaenda sehemu yenye amani au furaha ila ni kwa taabu na mateso hivi dahh..haya bana
Binadamu ana mifumo 11 ya kibaiolojia inayoongoza mwili wake. Mojawapo ni mfumo wa fahamu.
Mtu anapofariki, mifumo hiyo inakoma kufanya kazi, hivyo hatuwezi kutarajia mtu anayefariki afanye mambo ya kawaida, mifumo inamisbehave.
 
"1. Mara utaingia motoni, mara peponi. Nani amewahi kwenda kule? "​

"2. Kama ulivyokuwa hujijui ulipozaliwa, ndivyo itakavyokuwa utakapokufa."
Swali: We umejuaje itakavyokua utakapokufa, umewahi kufa?
 
Back
Top Bottom