hakuna haja ya kuwa na adhabu kama hizi mashuleni...!!!!!!!!!!!

hakuna haja ya kuwa na adhabu kama hizi mashuleni...!!!!!!!!!!!

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
habari zenu wakuu..!!! poleni kwa majukumu ya hapa na pale!!
bila kwenda mbali, mimi ni mmoja kati ya wale wasomi kutoka shule za saint kayumba, yes saint kayumba. najua mwajua sababu ya shule hizi kuitwa vivyo. kwa kugusia tu, hii ni kwa sababu ya kutumiwa na watoto wa wakulima na wafugaji kwa wingi!

ndugu zangu, kwa karne hii tuliyofika mpaka sasa na maendeleo ya sayansi na teknolojia tuliyofikia, hakuna haja ya uendelezo wa adhabu za kale ambazo hazina tija kwa maendeleo ya mwanafunzi mashuleni! adhabu hizi zimekuwa hatari sana kwa upande wa mwanafunzi ikiwemo kupoteza uwezo darasani kimasomo, kuwa mtu wa uoga kila wakati kitu ambacho hupelekea mwanafunzi kushindwa kuwa mvumbuzi na mdadisi wa vitu fulani ambavyo vingeweza kuleta tija katika utendaji kazi katika taifa.

kwa mfano ndugu zangu, adhabu hii ya wanafunzi kubebeshwa matofali, hebu kwanza fikiria uzito wa tofali lenyewe, mbali ya hapo, madhara yake hasa moja kwa moja kwa mwanafunzi yatakuwa ni makubwa sana!!!!!!!!!!!!!!!
sasa mi swali la msingi ambalo mi huwa najiuliza ni je hawa waalimu ambao hupatiwa mafunzo vyuoni, je wao hufunzwa na hiki kipengele cha adhabu kali kwa wanafunzi? amawao wenyewe ndio hujtungia mitaala ya adhabu????

moja kati ya adhabu pendwa ya tofali ni hii..!
View attachment 111304
je mwanafunzi hapa anafunzwa nini??? nidhamu ama ubabe?


adhabu hizi pia huwa ni udhalilishaji kwa mtoto wa kike ndugu zangu!!!

View attachment 111305View attachment 111306

hizi ni moja kati ya adhabu katili sana ambazo hupewa wanafunzi wa shule za msingi na mpaka wengine wa sekondari.......



je, serikali inalichukuliaje swala hili mpaka sasa??????????????


TUJADILI!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom