Hakuna Kama "KAMANDA" inatakiwa ipewe tuzo ya wimbo bora ya muda wote

Hakuna Kama "KAMANDA" inatakiwa ipewe tuzo ya wimbo bora ya muda wote

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
"Siku mapigo yangu ya moyo mwisho yatapogota,
Nuru itazima mfano wa Nyota inavyodondoka,
Sitaweza kuamka tena macho yangu yatapofumba,
Safari imewadia naenda kwa baba muumba,
Masela nawaachia usia,
Waambie ndugu na jamaa wapunguze kulia,
sote tutakwenda bali mimi ninatangulia,
Duniani siyo makazi yangu tena,
Niombeni kwa mola anilaze peponi pema,
Hamtaniona tena milele,
Nawaachieni majonzi tele,
Buriani naaga na nakata kauli,Roho yangu inatolewa na israeri,
Yowe la uchungu litasikika ,pale roho yangu itakapokuwa imetoka,
vazi langu sanda nitakuwa nimevikwa,Nipo kwenye jeneza tayari kwenda kuzikwa,
Mauti pindi yataponikabili,ni nani atakayeliziba pengo hili,
Uhai utabaki mzunguko wa damu umesimama,
Kama jahazi kina nilinazama,"


Nimeanza na kibwagizo tu kidogo ila zamani ilikuwa Moto ,

Hii ngoma hakika inahitaji ipewe tuzo ya Nyimbo bora ya muda wote ,
Ni moja ya Ngoma kali sana ya muda wote ilipigwa jana,leo na ata kesho ikifika itapigwa
Walioifanya hii Ngoma Daz Nundaz hakika walikaa wakafanya kitu siyo bla blaa tu,

Ngoma mashairi yamesimama,ukija kwenye biti nayo imepigwa kwa mpangilio mzuri sana kuendena na ngoma yenyewe,


Hakika mi nasema Hakuna kama KAMANDA..

Ayoo,siku mapigo yangu ya moyo yatapogota,
nuru itazima kama ndoto inapodondoka,
Sitaweza kuamka tena macho yangu yatapofumba,
Safari imewadia naenda kwa baba Muumba
Masela nawaaachia usia,
Waambie ndugu na jamaa wapunguze kulia
Sote tutakwenda bali mimi ninatangulia
Duniani sio makazi yangu tena,
Niombeeni kwa mola nilazwe peponi pema,
Hamtoniona tena milele,
Nawaachieni majonzi tele,
Buriani naaaga na nakata kauli,
royo yangu inatolewa na Isiraeli
Yowe la uchungu litasikika,
Pale roho yangu itapokua inatoka,
Vazi langu sanda ntakuwa nimevikwa,
Nipo kwenye jeneza tayari kwenda kuzikwa
Mauti pindi yatakaponikabili,
Ni nani ataeliziba pengo hili?
Uhai tamati mzunguko wa damu umesimama,
Kama jahazi kinani linazama
Buriani naaga masela,
Kwaherini ndugu jamaa na masela

Sa usingizi wa kupoteza uhai waninyemelea
jasho la hofu mwilini lanitiririka,
Naangaza kiza mwangaza,
napata kivuli cha mshumaa,
Malaika mtoa roho anisogelea,
miamba inagongana dhoruba,
tetemeko ngurumo mithili ya radi,"Ooh my god"
Roho huruma anachomoka,
chavuma kimbunga,najisi mwiko kuvunga,
Kwa shingo upande jalada la uhai nafunga
Ghafla fahamu nazingwa na utandu ukungu,
Shazingwa na ndugu kinywa chatema usia kwa mafungu,


Aamualo mola wala hawezi kosea,
Narudi udongoni nilipotokea,
kwa nguvu za mwenyezi ntatokea usingizini,
Nikiwatoka basi Yarabi yu kazini,
Uhai bado nautamani,
Ila sipaswi kubaki duniani,
Safari ya ahera ishafikaa,
kwaherini masela ndugu na jamaa,
Mja rudi mola wako kama umepotea,
Kumbuka ahera ndio unakoelekea,
Anza kutenda mema kabla kifo hakijakukuta,
Ukipuuza haya we utakuja kujuta


SAfari yangu sasa imeshawadia,
Kurudi kwa baba yanipasa naaga dunia,
Mwili umenyong'onyea,Viungo vimelegea,
Fahamu nimeshapoteza nimezingirwa na giza,
Milango yangu ya fahamu ishafunga
Kamanda naupoteza uhai nalamba mchanga
Umeshawdia wasaa pumzi nakata tamaa,
Na israeli roho yangu ndio anaitwaa,
Maandiko ya baba sasa yashatimia
na huko ahera sijui wapi ntafikia,
Jama naomba mnisamehe makosa yangu niliyotenda,
ili nipate makazi mema huko nakokwenda,
Kiroho nipo nanyi kimwili sipo tena,
Fateni yale mema niliyofanya na kusema,
Kwa huzuni nawaaga tena sirudi
NAsindikizwa na marashi ya ubani na udi,
Kwenye kaburi mtanihifadhi,
Na mbinguni ndio yangu milele makazi,
Maombi yenu ndio yatayoniponya,
Ili moto wa jehanamu nisijeuona,
Buriani naaga masela,
Kwaherini Ndugu jamaa na masela,
 
Nahisi kuna KAMANDA unayomaanisha wewe na sio unayotaka tufikirie
 
Ulikuwa wimbo mzuri..ila wa kupewa tuzo hiyo??? Hapana.
Aamualo mola wala hawezi kosea,narudi udongoni nilipotokea,
Kwa nguvu za mwenyezi nitatokea usingizini,nikiwatoka basi yarabi kazini,
Uhai bado nautamani ila sipaswi kubaki duniani,.
 
"Uhai bado nautamani ila sipaswi kubaki hapa duniani". Kila nikisikiliza wimbo wa Kamanda ikifika kwenye huu mstari nachanganyikiwa kwa woga nakosa furaha kabisa.
 
Hizi nyimbo zilikuwa on fire sana, yaani hata mistari ukiisikia unaona inavyotiririka na ujumbe. Sio kama currently songs.
 
Back
Top Bottom