Hakuna kilele kingine cha mafanikio usipokuwa na furaha, ichague leo

MUWHWELA

Senior Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
167
Reaction score
238
Habari za kuona siku hii Tena mpya, niwasalimu kwa pendo la dhati kabisa.

Nini hasa HATIMA ya Kila kitu Ukiwa hapa ulimwenguni,ukianza kupata majawabu ya haya Maswali yako utaanza kufunguka taratibu na hatimaye kuwa MTU HURU kabisa.


Binadamu anahitaji nini Ili awepo?je huyu binadamu Ili awe na furaha anahitaji nini? Je huzuni ni sehemu ya takwa au ni uchaguzi (option)ya MTU?

Kuna mambo matatu tu ambayo yote matatu HATIMA yake Haina UHAKIKA,haijulikani na kama inajulikana basi imeletewa SIASA ya fasihi ambayo Iko very corrupted

1-BINADAMU ANAHITAJI NINI ILI AWEPO,SIYO AENDELEE KUWEPO -Yaani hata ufanye BIDII ya namna Gani Bado viungo vya Mwili vitachoka na utarudi kwenye aina nyingine ya mtililiko ,Ukiwa kwenye frecuency hiyo hutapata kumbukumbu ya pale uliishi Ukiwa na Mwili,hii ni sheria ya Asili Haina mjadala.

Ilipaswa Kila anayezaliwa ajue na akumbushwe kwamba kuzaliwa ni chanzo au mwanzo wa kuelekea kwenye frecuency nyingine ambayo utaungana na viumbe wengine wenye uwezo wa kutambua na kuhimili frecuency hiyo. Hii itasaidia sana MTU mwenye mwili kuwa humble (mnyenyekevu)maana HATIMA yake haipo Katika utawala wake.

2:MTU KUWA NA FURAHA - Uwe unataka au hutaki ,ukishakuwa na Mwili basi lazima uchague furaha, maana usipochagua furaha mfumo wa Dunia utakuchagulia huzuni,masikitiko na shida.

Ukitazama vizuri furaha ni jumla ya utambuzi wa dhumuni la uwepo wako hapa ulimwenguni, dhumuni Hilo Halipo kwenye vitu, lipo kwenye Hali ya MAHUSIANO Yako na viumbe wengine.

3: MTU KUWA NA HUZUNI: Mtu kuwa na huzuni ni uchaguzi wake,maana huzuni nyingi ipo kwenye KUKOSA vitu siyo UTU.


Hatimaye MTU anakosa amani kwa sababu tu hana hiki Wala kile,je ukivipata vyote vitabadilisha HATIMA? Jibu ni hapana

Katika maisha yako Ndugu pata majawabu ya haya mambo matatu then ISHI Iko siku utaona maana ya maisha, don't be stressed na vitu..sisi kwetu furaha ndiyo gift pekee tuliyonayo.

HAKUNA KILELE KINGINE CHA MAFANIKIO USIPOKUWA FURAHA,CHAGUA FURAHA.
 
Asante sana.

Hiyo namba 1 sijaelewa vizuri.
 
Asante sana.

Hiyo namba 1 sijaelewa vizuri.
"Ili awepo ,siyo AENDELEE KUWEPO" huenda hii ndiyo imeleta confusion kwako ndugu yangu.

Vita yetu ni kupigania uwepo wetu Katika kipindi chote Cha ukomo wa viungo vyetu si zaidi ya hapo...Ili uendelee kuwepo lazima uwe mwenye Imani ya reincarnation (kwamba tutaishi Tena Katika mfumo Mwingine ) which is siyo tabu Yako leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…