Hakuna kitu kinaumiza kama unaamka Asubuhi na hujui utaenda wapi

kwaku the traveler

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2023
Posts
218
Reaction score
586
Yaani unaamka halafu hauna mishe zozote au mishe ulikuwa nazo zinegoma aisee inapain sana.

Nilipitia hii hali basi bwana nilipopanga chumba unaona vyumba vya majirani zako Wanaamka Mapema wanaenda mishe kurudi jioni Mimi nipo tu

Hii hali ilinitesa sana kutokuwa na mishe full no respect mtaani yaani unaona kabisa hapa hii kwakuwa sina mishe

Basi bwana, nikaona nisiwe boya nikaanza nami kuamka mapema naoga na vaa vizuri naondoka kumbuka sina kazi yoyote hapo naenda mjini

Naenda zangu mjini kuzurura kumbuka kama hauna mishe jua linachelewa kuzama hatari

Mimepiga hiyo kitu kama miezi mitatu heshima nilipokuwa nakaa ikarejea kidogo, mabinti walikuwa wengi hapo napoishi wakawa wananiambia eeh sikuizi umepata mishe hongera Mimi najibu si unajua tena, kumbe wangejua nazurura tu mjini huko

Nifupishe, katika kuzurura kwangu nikapata Dili hilo Dili ikanipa Hela kidogo hiyo Hela nikaona fursa huko huko mjini nikatembea nayo

Tutoke maghetoni vijana Dunia Haina huruma na mtu asiyekuwa na shughuli ya kumwingizia kipato

Kama ushapitia hali hii pita hapa toa experience yako ilikuwaje

Mungu awapiganie Wote wanaoamka Asubuh halafu sehemu ya kwenda hawana wapate mishe๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ
 
Kama ushapitia hali hii pita hapa toa experience yako ilikuwaje
Ilaa mwanangu ukikosaa mishe ,ujue pia nayo n mishe hatari zaidii ๐Ÿ˜‚,,

Ctk hata kukumbukaa 2018 na nikagongewaa na dem wangu niliyekuwa naishi naye na tuna mtt mmojaa kisaa kukosa helaa tu hata ya kulaa ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…..na ndio hapo moyo wakupenda Tena ulikufaa kifo Cha wazi maninaaa ,Leo hii uniambie nn kuhusu mapenzi nikuelewe manina mm ...oyaaaaa umaskini n mbayaaa zaidi ya ukimwi
 
Hahhaha dah aisee mbona ilikuwa hatari
 
Haijawahi kutokea othewise naumwa mkuu!

Labda kama akili yako ni mgando ....Dar nilikuja bila ramani wala connection lakini sikuwahi kukoswa kazi,Dodoma pal;e nilikaa siku2 tukaanza kuchimba mitaro.

Na uhakika unasubiri kazi za ofisini mkuu
Hamna Mzee si unajua umetoka zako chuo mda huo afu umeingia mtaani mtaa unakukataa Hila mungu mkubwa saiv nikiamka najua naenda wapi
 
Jaribu kufikiria wale jamaa walikuwa under ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ AID, juzi kuna jamaa waliandaliwa kwenda nyanda za juu kusini kupiga kazi, walishaandaa mambo yao, perdiem za kutosha. Mara paap, safari imesitishwa. Ile miradi iliyopo chini ya USAID yote imelala, zile NGO zilizopata kuendesha miradi chini ya marekani...noma na nusu!
 
Uko sawa 100%
 
Hiyo Hali uisikie tu kwa mpita njia akihadithia. Tena ina unafuu ukiwa gheto kwako, vuta picha ile unakaa kwa broo halafu shem ni mnoko sana. Anamka asubuhi anakuambia sehemu mi Leo sipiki kwahiyo utamalizia hicho kiporo Cha wali na maharage.
Ukila ukishiba inaomba Mungu isipite hali yoyote ya uchafuz wa hewa maana shemej yako atajua wewe ndo umeharibu Hali ya hewa, na huwez kukata maana wewe ndo umeshindia kiporo Cha wali maharage
 
Nafikiri kutoka asubuhi na kwenda kuzunguka uwe na au huna kazi sio guarantee kwamba unaingiza kipato cha maana.
Kuna watu hatutoki na hela zinanifuata hapahapa.Hii akili ya kwamba kupata hela lazima utoke alfajiri urudi jioni ni outdated.
Jifunze kuendesha maisha kwa namna ambayo hata ukiumwa ukalala chini hela zitaingia tu
Mambo ya mtaa unakuonaje au unasemaje ni upuuzi huo.Cha msingi kuwa na pesa
 
Muhimu uwe na kitu kinachokuingizia kipato, hiyo ndio hoja ya msingi. Kuwa idle ni hatari hata kwa afya ya binadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ