Hakuna kukata tamaa💪💪💪

Faru01

Member
Joined
Jun 29, 2022
Posts
32
Reaction score
125
Nimeingia Dar juzi nimepata chumba Mbezi karibu na Stendi ya Magufuli katika harakati za kusaka tonge leo nimechanganya kwenye nikawa nauza maji hapa Mbezi stand ya daladala mgambo wakanikamata wakachukua mzigo nimerudi geto kulala, naombeni idea mishe gani nipige hapa town nisikose hela ya kula.

 
Hii sheria kandamizi sana! Kama wamezuia mtu asifanye biashara maeneo hayo kwa nini wachukue mtaji wa mtu? Huku ni kurudisha nyuma harakati za vijana kujikomba!
 
Mkuu hizo Sandals zako, nimemiss kuvaa pamoja na rubega nikienda Umasaini kusalimia.
 
Dah,pole Sana mkuu, laana ya Mungu iwe juu yao hao mbwa
 
Dah! Bora urudi tu Kijijini tulime. Tena msimu kama huu karibia maeneo yote nchini yanavuna chakula. Hivyo hakuna njaa! Ya nini kuteseka ugenini kama mwana mpotevu?

Kumbuka jembe halimtupi mkulima.
 
.......daah! pole sana mkuu ndo maisha ya mwanaume hayo, simama tena, ingekuwa betting tungesema next time stake what you can afford to loose, sasa hii ya kuporwa na mgambo sijui tuiite nini.......
 
Hii sheria kandamizi sana! Kama wamezuia mtu asifanye biashara maeneo hayo kwa nini wachukue mtaji wa mtu? Huku ni kurudisha nyuma harakati za vijana kujikomba!
na wewe kama umezuiwa kufanya biashara eneo hilo kwa nini unaendelea kuhatarisha mtaji wako kwa kukaidi amri?

It goes both ways my dear
 
Zama ndichi chukua dawa tembeza kwa wadau kimya kimya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…