SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Niliongea na tajiri Mo akanisikiliza. Tajiri alikuwa kachafukwa. Aliona dharau zimezidi mtaani. Kaenda Uarabuni kabeba chuma kingine.
Simba misimu hii miwili imechukua wachezaji wawili ACTIVE kutoka timu za Uarabuni, tena timu kubwa. USMA ndiyo wale waliwapiga mabomu vyura usiku na mchana na wakawafunga vilevile, vyura wakabaki kuringishia medali za shaba. Simba ilimchukua Super Coach Benchikha pamoja na kwamba kipindi chake hakikuwa kizuri sana lakini hiyo ni habari nyingine.
Tulihitaji striker, tumeenda Uarabuni tumevunja mkataba. Hakuna Leonel boya. Hayupo! Awesu ndani, Kagoma ndani, Kijili ndani, Leonel Ateba ndani, MVP wa Nigeria ndani, MVP wa Ivory Coast ndani, mfungaji bora ligi ya Ghana ndani, hii kweli ubaya ubwela.
Kwa kumalizia, waonyeni wachezaji wakae mbali na wachezaji wa Yanga. Haijalishi una historia gani na hiyo chura inayofanana. Haijalishi mnatoka nchi moja, kaa mbali na vyura, itakusaidia wewe na itatusaidia sisi. Waambie waweke PAUSE ya mawasiliano na hao watu kwa misimu miwili tuna jambo letu. Mkikutana mnapeana hi mnagonga ngumi maisha yanaendelea. Tuko vitani hatucheki tena na kima.
Ooh, Mo boresha pia idara ya utabibu na afya hapo Simba, napo naona kuna shida kubwa. Sijajua ni uhaba wa vifaa, wahudumu au nini ila napo panahitaji kufanyiwa kazi kubwa. Hatuwezi kuendelea kuacha wachezaji wakipata tu majeraha.
Soma Pia: ATEBA ni Mnyama, Asaini miwili msimbazi
Sina ninalowadai wote waliohusika katika zoezi zima la usajili. Mmetisha sana. Tukutane uwanjani.
Ubaya Ubwela!