Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Mwaka 2022 Mahakama ilibatilisha kifungu cha 11 (1) (c) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kinachoweka zuio kwa wafungwa wanaotumikia adhabu ya kunyongwa na wanaotumikia adhabu ya kifungo cha zaidi ya miezi 6 kujiandikisha ili kupiga kura.
Hivyo kwa kufuta kifungu hiki ilifanya wafungwa wote wa makosa ya kawaida ya jinai kuwa na haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu bila kujali muda ambao wametumikia gerezani.
Hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Elinaza Luvanda inatokana na shauri la Kikatiba lililofunguliwa na raia wawili; Tito Magoti na John Tulla ambao walikosa haki ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kutokana na kuwa mahabusu (japokua Sheria ilikua inakataza wafungwa na sio mahabusu) ambapo walidai kuwa kifungu hicho kinakinzana na Katiba Ibara ya 5(1) ambayo inaeleza kuwa kila raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 anayo haki ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu.
Sheria mpya ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024 imeendelea kuwa na kifungu hiki kilichobatilishwa na Mahakama kwa kuendelea kuwanyima haki wafungwa kushiriki katika uchaguzi kwa kuwa hawana vigezo vya kujiandikisha kupiga, ambapo Kifungu cha 10(1)(c) kimesema wafungwa waliokuhumiwa kifo au kifungo zaidi ya miezi 6 hawatakuwa na haki ya kupiga kura!
Hivyo basically hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika kwasababu hata mwanzo wanaotumikia kifungo cha chini ya miezi 6 walikuwa bado na haki ya kupiga kura. Serikali imeendelea kukaidi amri ya mahakama iliyobatilisha kifungu kinachomzuia mfungwa kupiga kura (wakati Haki hiyo imetolewa kikatiba) na kukirejesha katika Sheria mpya ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani chini ya Kifungu cha 10(1)(c) kinachozuia wafungwa kujiandikisha na kupiga kura.
Pia soma: Makalla: Wafungwa chini ya miezi sita (6) watapiga kura Uchaguzi Mkuu
Hata Kifungu cha 42 ambacho anasema kinamruhusu kila mtu kupiga kura
kimewekewa kizingiti/kigezo kwamba lazima mtu awe amejiandikisha, lakini huwezi kujiandikisha kama hujakidhi vigezo, na kigezo kimojawapo ni kwamba hutakiwi kuwa mfungwa wa adhabu ya kifo au mfungwa wa zaidi ya miezi sita, sasa hii inamaanisha hamna mabadiliko yoyote makubwa yaliyofanywa au hata madogo kuhusu ushiriki wa wafungwa kwenye uchaguzi wa Urais kama anavyotupanga.
Team chawa ukiongozwa na mama anatosha Lucas Mwashambwa ChoiceVariable Tlaatlaah johnthebaptist mbebe na wenzenu mjeeee
msisahau kumbeba mwanasheria Pascal Mayalla awasaidie kusoma maandishi kwa uzuri

yaani siku hizi ni mwendo wa kububujikwa machozi ya huzuni tu... kila mnapogeuka mnalabuliwa... lazima mkae mguu sawa saivi