Hakuna malaria lakini ana joto

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
3,023
Reaction score
1,315
Mwanangu ana miezi 11.Anachemka na kuharisha tumepima malaria hakuna.Atakuwa ana tatizo gani?
 
Mpeleke hospital Dr atamwona na kujua anaumwa nini, acha kutibu kienyeji utaua mtoto. Watoto wako very delicate
 
Mpeleke hospital Dr atamwona na kujua anaumwa nini, acha kutibu kienyeji utaua mtoto. Watoto wako very delicate

Agreed!! Kuna sababu nyingi sana za homa (joto) kwa watoto na sio malaria peke yake. Ni vema kumpeleka hospitali akafanyiwe uchunguzi wa kina kubainisha shida ni nini ili mtoto wako apate tiba stahili!
 
kwan hilo ndo la kuomba ushaur?we nenda kwa dr then utasaidiwa zaid kwan anatampima na kugundua tatizo.tena fasta fanya uende
 
Pamoja na kumuona Dr. Pia mpime mtoto UTI, madaktari wengi husau hii kitu wakati ni very common kwa watoto
 
Mpime malaria sehemu tatu tofauti na UTI february nusu nimuue mtoto wangu nimepima naambiwa hamna malaria kumbe anamaria kurudi home mtoto akazidiwa mpima malaria sehemu nyingine 2 mtoto ana malaria 3 ningempoteza lol
 
Fuata ushauri wa Nivea. Pia kama unaridhika kuwa mtoto anazo dalili za malaria tafadhali hakikisha anapata tiba ya malaria bila kijali kama imeonekana au la! Nimepata uzoefu huo mtoto alilazwa siku tano pima vipimo vyote joto linapanda mbaya. Malaria haionekani etc. Wakati huo alikuwa anaangaliwa na jopo la madaktari...Dr mmoja baada ya option zingine kuwa hakuna akaamua apewe dozi ya malaria. Mtoto alipata nafuu na kupanda kwa joto kukaishia jumla.
 
kwan hilo ndo la kuomba ushaur?we nenda kwa dr then utasaidiwa zaid kwan anatampima na kugundua tatizo.tena fasta fanya uende
Nojo, unakuwa kama huwafahamu wauguzi wa TZ! Mtoa hoja anaomba ushauri si kwa sababu hajui/hajafika hospitari, bali kapata matibabu yasiyolidhisha; wauguzi wanakimbizana na ugumu wa maisha na hakuna uhakika wa matibabu!

Kwa mtoa hoja, joto ni kiashilia kwamba mwili wa mtoto unapambana na 'infectious bacteria'. Joto likiongezeka hadi 37.8^C ina maana kinga ya mwili inauwezo wa kupambana na 'infection' husika na si lazima sana kutafuta matibabu. Likivuka 38^C inaashilia kinga ya mtoto imezidiwa na hunabudi kumwona daktari. Tatizo kwa kesi yako ni kwamba viashilia vya joto na kuharisha ni ishara ya matatizo mengi, hivyo usichoke kumfanyia uchunguzi hasa UTI, tumbo, sikio na koo.
 
inaweza kuwa infection yoyote katika mwili sio lazima malaria watu wengi tunafikiri joto la mwili kupanda ni malaria joto la malaria lina kiwango chake pia lakini infection inaweza kupandisha hata mpaka 40 na hapo ndipo mtoto anawezapatwa na ile kitu inaitwa degedege na hata kupoteza maisha ua kuleta tatizo katoka ubongo hivyo kuja kumfanya mtoto kuwa na kumbukumbu ndogo au hata tahaira kabisa.

Kama mtoto anapata UTI na ni wa kiume solution yake ni kumtahiri pia kujitahidi sana kumweka kaika mazingira masafi, haswa kama ni wa kike pia hawa wakinadada tunawaachia watoto wengi wao hawajui kuwatunza watoto au wengine hawajali na wengi wao tumewatoa vijini hawajali sana swala la usafi kwa mtoto hii mara nyingi hupelekea mtoto kutapa UTI.

Pia ni vizru kuhakikisha unapima malaria hata mara mbili kwa sehemu mbili tofauti hawa wataalamu wetu wa maabara nao wakati mwingine ni binadabu kama wengine na wengine sio makini kwenye kazi yaani wazembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…