Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,606
- 1,711
Baada ya shutuma kali kuhusu dhana ya kwamba mapenzi bila pesa yamekufa sasa nimerudi na dhana ya mapenzi bila kuaminiana yamekufa. Ndio. Love without trust is dead. Au ukipenda unaweza kuiweka hivi: No trust, no love. Yaani: Bila kuaminiana, hakuna mapenzi. Hapa hatuongelei kuaminiana kwa 90% au 99%. Tunaongelea kuaminiana kwa 100%. Ukishapoteza tu hata 1% hesabu kuwa hakuna penzi hapo. Mfano mrahisi wa kuaminiana 100% ni huu:
Dada mmoja alipoambiwa kuwa kuwa mume wake kambaka na kumuua mwanamke fulani basi alienda korokoroni na kumuuliza mume wake hivi: 'Wanasema umefanya kitu kibaya kwa mwanamke fulani'. Mume akajibu: 'La hasha';. Mwanamke akamkumbatia mume wake kwa imani kisha akaondoka. Baada ya kukutana na jirani yake ambaye alimchongea huyo mume, mazungumzo yakawa kama ifuatavyo. Mke: 'Mume wangu hana makosa'. Jirani: 'Una uhakika gani?' Mke: 'Ameniambia'. Yaani hii ni imani thabiti isiyotetereka na ndio msingi mkuu wa mapenzi.
Pamoja na hayo yote, hii haimaanishi kuwa zile 'p' ama 'k' 3 za msingi katika mapenzi hazihusiki. Zinahusika sana. Tena zina uhusiano mkubwa na kuaminiana. Ukiona mwanamke haamini kuwa unaweza kum-p/kum-k hakuna penzi hapo. Fungasha virago. Kama vipi basi jaribu kurudisha kuaminiana. Ila hiyo ni kazi ya Kihekuli kama si ya kisisifi.