Hakuna Mapenzi bila Kuaminiana 100%

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,606
Reaction score
1,711
Baada ya shutuma kali kuhusu dhana ya kwamba mapenzi bila pesa yamekufa sasa nimerudi na dhana ya mapenzi bila kuaminiana yamekufa. Ndio. Love without trust is dead. Au ukipenda unaweza kuiweka hivi: No trust, no love. Yaani: Bila kuaminiana, hakuna mapenzi. Hapa hatuongelei kuaminiana kwa 90% au 99%. Tunaongelea kuaminiana kwa 100%. Ukishapoteza tu hata 1% hesabu kuwa hakuna penzi hapo. Mfano mrahisi wa kuaminiana 100% ni huu:

Dada mmoja alipoambiwa kuwa kuwa mume wake kambaka na kumuua mwanamke fulani basi alienda korokoroni na kumuuliza mume wake hivi: 'Wanasema umefanya kitu kibaya kwa mwanamke fulani'. Mume akajibu: 'La hasha';. Mwanamke akamkumbatia mume wake kwa imani kisha akaondoka. Baada ya kukutana na jirani yake ambaye alimchongea huyo mume, mazungumzo yakawa kama ifuatavyo. Mke: 'Mume wangu hana makosa'. Jirani: 'Una uhakika gani?' Mke: 'Ameniambia'. Yaani hii ni imani thabiti isiyotetereka na ndio msingi mkuu wa mapenzi.

Pamoja na hayo yote, hii haimaanishi kuwa zile 'p' ama 'k' 3 za msingi katika mapenzi hazihusiki. Zinahusika sana. Tena zina uhusiano mkubwa na kuaminiana. Ukiona mwanamke haamini kuwa unaweza kum-p/kum-k hakuna penzi hapo. Fungasha virago. Kama vipi basi jaribu kurudisha kuaminiana. Ila hiyo ni kazi ya Kihekuli kama si ya kisisifi.
 
Usanii uliopo kwa kizazi cha sasa cha ambapo maneno 'dot' na 'com' yamekuwa chanda na pete; sitakosea nikonkudi kuwa mahusiano ya sasa ni kufanya ngono tu na kuanzisha familia, right?
 
Usanii uliopo kwa kizazi cha sasa cha ambapo maneno 'dot' na 'com' yamekuwa chanda na pete; sitakosea nikonkudi kuwa mahusiano ya sasa ni kufanya ngono tu na kuanzisha familia, right?

nahisi ulishakata tamaa kuhusu kuaminiana 100% zamani, nami nashawishika kuhitimisha 'ewe mwenye imani haba'!
 
nahisi ulishakata tamaa kuhusu kuaminiana 100% zamani, nami nashawishika kuhitimisha 'ewe mwenye imani haba'!

U r right, ninaye muamini hiyo 100% ni Me, Myself n I tu. I am a victim of my own experience!
 
U r right, ninaye muamini hiyo 100% ni Me, Myself n I tu. I am a victim of my own experience!

then all the best with pragmatic love which, in essence, is not love at all
 
ili uenjoy penzi lako unapaswa umuamini mwenzio.....
na kwenye mapenzi lazima utake risk....ndo risk yenyewe hiyo....
 
u cant trust anyone 100% coz to trust someone 100% that means they're perfect and we all know no one is perfect. Its hard to trust your own family 100% let alone your partner.
 
u cant trust anyone 100% coz to trust someone 100% that means they're perfect and we all know no one is perfect. Its hard to trust your own family 100% let alone your partner.

no. you don't need someone to be perfect to trust him/her.

yes. you can trust hence love. it is hard. but not impossible.
 
wakati mwingine kumhisi mtu bila ushahidi humsukuma kwenye kuvunja uaminifu!
nakuunga mkono mara nyingi tunapenda kuishi under assumption ambayo siyo nzuri kabisa ku assume mwenza wako yuko hivi wakati hayupo hivyo...............mwisho wa siku unafanya maamuzi ambayo haukuyatarajia na kuja kuyajutia baadaye kutokana tu................na kuhisi kitu ambacho hauna ushahidi nao.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…