'Hakuna Masikini Jeuri, Na ukiwa Maskini Jeuri utakuwa Maskini milele' Zamaradi afunguka

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304

HUTAKIWI KUWA NA HASIRA KATIKA PROCESS ZA KUTAFUTA MAISHA.... utakutana na changamoto nyingi sana na lazima ukubali.. kubali kudharauliwa, kubali kushushwa kubali kuonekana huna maana lakini lengo ni ufikie pale ambapo siku moja kila mtu atakuheshimu..

Lakini ukianza kuchukulia kila kitu personal, kuwa na vinyongo na watu na kukataa dharau za huku chini trust me HUTOFIKA POPOTE.. Ukitaka kuvimba kabla hujafika utachelewa.. wenye mivimbo wengi hawajafika mbali kwenye maisha.. kumbuka tu BOSS HANUNIWI!!! Huu msemo una maana kubwa sana pamoja na kwamba kila mtu anautafsiri kivyake.. lakini ni sawa na kusema tumikia kafiri upate mradi wako.. unachokihitaji wewe unakijua..

DHARAU zake ama chochote chake fanya kama hazikushughulishi.. maisha ni safari ndefu na hakuna aliewahi kuahidi kwamba itakuwa ni safari rahisi.. kubali vikwazo kama sehemu ya safari.. na wengi waliojishusha katika kutafuta tumeona matunda yao asikudanganye mtu HAKUNA MASKINI JEURI.. Na ukiwa maskini jeuri utakuwa maskini milele... ndivyo ilivyo na SI kwamba ni kitu kizuri ama kinasapotiwa.. la hasha!! Ila ndivyo maisha yalivyo.. wanasema LIFE IS NOT FAIR!!

Haikugharimu kuwa mpumbavu pale ambapo unaona kuna faida na wewe.. unachotakiwa kujua 'KUJIFANYA MPUMBAVU mbele ya mtu ANAEJIONA MWEREVU ni kumfanya YEYE mpumbavu bila kujua...' kumbuka tu usije ukatumia hii vibaya ukajikuta umekuwa MPAMBE badala ya mtu anaetaka kutimiza ndoto zake - Zamaradi.
 
Mawazo ya ki CCM CCM hayo, upuzi..
 
Ukiwa masikini hutakiwi kua jeuri. Mfano mzuri wachaga wakija mjini akifungua duka lake lazima wateja wajae dukani kwake ni kwasababu anaijua siri , ana lugha nzuri ya kumfanya mteja ajisikie anathaminiwa.
 
"Maskini jeuri huu ni msemo tu, huwezi kuwa masikini afu ukawa jeuri" Mwana Fa
 
translated in swahili...insipiring message though.
 
Wacha kutwambia wachaga wanaoenda mwezi akumi na mbili ku renew matambiko.
 
Zamaradi yuko smart sana kichwani, ni baadhi ya mastaa wachache wanaojiamini na kujitambua...i like her
 
Ukiwa masikini hutakiwi kua jeuri. Mfano mzuri wachaga wakija mjini akifungua duka lake lazima wateja wajae dukani kwake ni kwasababu anaijua siri , ana lugha nzuri ya kumfanya mteja ajisikie anathaminiwa.

Ar you among chagaz!?
 
Zamaradi yuko smart sana kichwani, ni baadhi ya mastaa wachache wanaojiamini na kujitambua...i like her

Angekuwa smart kama unavyomsema asingemzalia ruge mtoto. Kwangu ni mtu average kama wanawake wengine tu.
 
Ndio maana akamvulia chupi BOSS wake Ruge ili apate atakacho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…