Hakuna mfanya biashara aliyeporwa fedha zake, kuwarudishia ni mbinu nyingine yenye ufisadi na viongozi kutengeneza biashara zao wenyewe!

Serikali imekuwa mahakama.?

Mashahidi ni kina Nani Kwa wakati huo mkuu,

Si ni rahisi tu mlalamikaji kusema aliporwa bilioni kadhaa ilihali kumbe ni million moja tu
Ndo maana nikasema serikali haikufata utaratibu wa kuzichukua hizo fedha na leo watu wanaweza wakatumia huo mwanya kufanya ufisadi. Kiongozi asiyesimamia taratibu na sheria za nchi yake mwenyewe hafai sababu lazima ataleta shida tu mbeleni na mambo ya fidia au mambo kama haya. Hawa watu wangekamatwa, wakafunguliwa mashtaka ya ukwepaji kodi, kesi ikasikilizwa, wakahukumiwa leo nani angekuja kusema walipwe?
 
Mkuu hatuwezi tuliowengi hatuwezi kukuelewa lakini huo ndiyo ukweli mchungu, mazingira harali na kipato harali ndiyo yaliyotengenezwa, Tutahitaji nguvu kuishinda nguvu hasi
 
Unadhani mkuu, malalamiko tu ya mtu yeyote yatoshe kulipwa fidia?

Embu fikiri kwa upya
Mkuu watu walinyang'anywa mali zao bila amri za mahakama, bila uthibitisho kwamba hawalupi Kodi. TENA WENGI WALIKUWA NA TRA CLEARANCE FORM KUTHIBITISHA HAWADAIWI, Sasa serkali inataifishaje Mali ya mtu bila amri ya mahakama?? Mfano nikuulize wale watu wa bureau de change walinyang'anywa fedha na Mali zao chini ya sheria ipi??
Na pia wengine acount zao zilitolewa fedha as if ni magaidi, bila maelezo yoyote.

ISTOSHE HATA VIONGOZ TUMESKIA MALALAMIKO WALITAMAN MAKI ZA WATU WAKAZICHUKUA KIBABE, YANI MADIWANI, DC, RC NAO WALITUMIA MADARAKA YAO VIBAYA KUJIPATIA MALI.

HAWA WAATHIRIKA HAWAFIDIWI, BALI WANARUDISHIWA MALI ZAO
 
Serikali ikianza kulipa tu fidia kwa sabb kuna watu wamelalamika kuporwa na serikali hiyo, bila mlalamikaji kwenda mahakamani na mahakama ikajiridhisha, huo ni ufisadi tuu hakuna jina lingine zaidi ya hilo
Wao wakati WANACHUKUA fedha za watu mabenki huko na bureau de change walienda mahakamani?? Watu wapewe Mali zao walizotafuta Kwa jasho
 
Mkuu yaan Mimi nimemaliza la Saba, Kwa ukiritimba wa serkali yangu makosa nafasi ya kwenda form one, baadae mzaz wangu anapata mahali mtoto aliacha shulena haonekani, napelekwa Mimi nikarudie darasa na naambiwa na mzazi wewe kuanzia Leo utaitwa hivi, Sasa nakataaje?? Ni kosa langu Mimi mtoto ama ni kosa la serkali na mzazi??

ISTOSHE MIMI NAKAA DARASANI, NASOMA KWA BIDII NAFANYA MITIHAN NA NAFAULU KWA AKILI ZANGU. SASA HICHO CHETI CHANGU HAPO KINA UFEKI GANI?? WAPI KWENYE SHERIA ZETU NAKATAZWA KUBADILI JINA??

MAANA YAKE NI KWAMBA UTAALAM NA USOMI NIMEUSOTEA MWENYEWE NA MIMI SIO KILAZA, BAS TU MLIDHULUMU WATU WALIOWATUMIKIA KWA MOYO NA NGUVU ZAO
 
Utakoma ulizoea vya mteremko sasa unaona faida ya ubabe.
 
Kwa taarifa yako mimi ni multi skilled person situmbuliki
Lazima utakuwa unatokea kwenye ukoo wa VILAZA , kama sio wewe uliepitiwa na fyekeo la Mwamba basi ni jamaa za ukoo wako.

Matapeli wote wana hio "multi skilled" ndo TUMA KWA NAMBA HII waleee.
 
Ni kweli hawakuporwa pesa na Serikali, waliporwa na Jiwe na mtu wake wa karibu, bwana mganga.

Kama wangekuwa wameporwa na Serikali, pesa ingeenda Serikalini. Pesa hiyo, CAG hajaiona mahali popote ndani ya hazina au taasisi zilizo chini ya Serikali.

Mwendazake alizipora pesa hizo kwa kutumia madaraka yake. Ni sawa na mtoto jambazi akaenda kwa majirani na mtutu wa bunduki, akawapora majirani pesa akidai kuwa anatekeleza maagizo ya Baba yake. Bahati, mtoto akafa. Baba akataka mahusiano mema na majirani. Pesa aliyopora mtoto kwa jina la Baba, hata haikumfikia Baba, lakini Baba akaamua kuwarudishia majirani zake waliokuwa wameporwa na mtoto jambazi.

Nadhani inachofanya Serikali ni sahihi kabisa, lakini pesa ile iliyoporwa na marehemu, lazima iko mahali. Marehemu hajaenda na pesa hiyo kaburini. Wakamatwe akina mganga ili waeleze hiyo pesa iko wapi.
 
Nenda mahakamani, na sio serikali ishughurikie malalamiko hewa

Nyambafu, simama kwenye hoja fisi wewe!
Kauli zako mbona inaonekana hupo timamu? Huwezi kuchangia mjadala kwa hoja thabiti? Kutukana ni dalili ya kupungukiwa akili. Punguani na vichaa, chunguza mwenyewe, jambo pekee ambalo pamoja na kupoteza akili, huwa wanaweza, ni kutukana.

Ukiona unapenda sana kutukana, ujitafakari sana. Ujipime kama bado ni mzima. Magonjwa ya akili, wengi huwa hawajitambui, na hata watu wa karibu wanaweza wasijue. Wengine huishia kusema, fulani siku hizi amebadilika sana, kumbe mwenzao amekwishaugua matatizo ya akili, hasa kwa wale ambao wapo karibu na mstari unaotenganisha wagonjwa wa akili na walio wazima.
 
Angalia wanaompinga mtoa mada utagundua akili za watanzania ni za ajabu kuliko binadam mwingine yeyote. Sasa mnampinga na kumkashifu ili watu walipwe tu bila utaratibu? Hivi kama mtu hajapeleka madai mahakamani akatambulika na kesi ikasikilizwa, serikali inaamuaje kumlipa tu mtu? Mnaopinga mlitaka serikali ilipe kwa utaratibu gani?
 
Mtoa mada unajifanya hujui kilichotokea awamu ya 5

Na utakuta wewe ulikuwa task force na ulishiriki kuchukua fedha kwa nguvu..

Kwanza task force mlichukua nyaraka zote, laptop/ computer.. Pamoja na kuharibu camera ili kusiwe na ushahidi..

Mnafilisi watu makusudi na wengine mkawapa magonjwa ya moyo..

Mimi sifurahii kifo cha mtu.. Na hakuna mtu yoyote atabaki hapa Duniani..
Lakini naomba niseme IT WAS A PERFECT TIMING KWA DIKTETA KUTUTOKA... na walimchelewesha sana...
 
Unadhani mkuu, malalamiko tu ya mtu yeyote yatoshe kulipwa fidia?

Embu fikiri kwa upya
Sidhani kuwa huku Serikalini kote hakuna wenye akili, yaani waamue tu kuwa tuwarudishie pesa zao.

Marehemu baada ya kuwabambikia kesi za uhujumu uchumi, kwa zaidi ya miaka miwili, alishindwa kupata ushahidi hata wa kutengeneza kuwa wale walikuwa ni wahujumu uchumi.

Baada ya kuwatesa kwa kipindi kirefu, akaishia kuwalazimisha kuwa wakiri makosa, na wakubali kulipa, na watakaokataa atawakomesha kweli kweli.

Kama walikuwa na makosa, ni nini kilichomfanya ashindwe kuendelea na kesi za kuwabambikizia aluzowapa?

Halafu pesa waluzolipa, akazipora yeye binafsi kwa manufaa yake. Ile ilikuwa ni blackmailing. Ni bahati tu Mama Samia ni mpole. Tukifuata haki, wale wote walioshiriki kwenye uporaji ule ilistahili wakamatwe, wafunguliwe mashtaka kwa uporaji wa pesa za watu kwa kutumia ofisi ya umma.

Uzuri, jinai haifi, lazima mganga na wale majambazi wenzake, **** siku watafikishwa mbele ya mkono wa sheria.
 
Serikali ikianza kulipa tu fidia kwa sabb kuna watu wamelalamika kuporwa na serikali hiyo, bila mlalamikaji kwenda mahakamani na mahakama ikajiridhisha, huo ni ufisadi tuu hakuna jina lingine zaidi ya hilo
Paulsylvester, tuanze na hili;

√ Je, ni kweli wote tunakubaliana kuwa serikali ilitumia nguvu ikiwemo jeshi la wananchi (JWTZ) kule Arusha kuchukua pesa kwa nguvu kwenye maduka ya watu ya kubadilishia fedha za kigeni na kwa mfanyabiashara yeyote aliyeonekana ana kiasi kikubwa cha pesa benki..?

Je, hukumbuki kuwa watu walifungwa magerezani kwa kisingizio cha ukwepaji kodi na mwisho ili watoke kwenye mateso ya gerezani walilazimishwa kutoa kiasi fulani cha pesa kwa kilichoitwa "Plea bargaining" ambayo ilikuwa kunyume cha utaratibu na sheria...?

Swali: Serikali yenyewe kwa kufanya vile wakati ule ilitumia mahakama gani iliyoruhusu iwafanyie watu uporaji ule..?

KWA MAONI YANGU:

1. Serikali imefanya vyema, kwani wakati inapora haikutumia mahakama na sasa irudishe fedha za watu kwa njia ileile...

2. Hizo siyo fedha za walipa kodi kama unavyodai. Tangu lini fedha ya kuibia mwenzako ikawa yako..? Kwa hiyo, ni vyema sana seeikali iwarudishie watu fedha zao ilizochukua kwa nguvu bila sababu za kufanya vile...!!

3. Wakienda mahakamani, watashinda kesi na itabidi serikali ilipe mara mbili na fidia juu. Kama mazungumzo yameshafanyika nje ya mahakama na ikaonekana walinyang'anywa pesa zao kwa uonevu tu bila sababu, kurudisha mali ya mtu huyo ni uungwana na ni haki...!

NOTE:
Tunachoweza kudai sisi ili kuondoa hayo mashaka uliyonayo ya baadhi ya viongozi wa serikali kutumia nafasi hiyo kuiba tena fedha ya umma, ni kuitaka serikali ifanye zoezi hili kwa UKWELI na UWAZI..

Yaani, majina ya wote wanaodai waliporwa pesa zao yawekwe wazi, kiasi alichoporwa na kinachorejeshwa kwake nk nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…