Hakuna "Mjenzi Huru", game ime-change tu

Broadcast

Member
Joined
Jun 19, 2022
Posts
76
Reaction score
285
Icon wa bongo fleva bwana Diamond Platnumz wengi wetu wanahisi kama ni mjenzi huru kutokana na maisha yake matanuzi yake mafanikio yake na endorsement zake.

Lakini cha kushangaza ukiachana na yeye kuna wasaniii wengi hapa bongo wana maisha mazuri na mafanikio mazuri tu ingawa sio ya kumfikia Platnumz

Muangalie Jux, Nandy, Konde Boy, Ali Kiba, Rayvan wote hawa ni baadhi ya wasaniii wana maisha mazuri tu lakn hatuwaoni kama wajenzi huru.

Ndo maana na hitimisha kwakusema hakuna cha ujenzi huru game ya mziki imebadilika.
 
NJIA RAHISI YA KUMJUA MJENZI HURU ANGALIA MASHAIRI YA NYIMBO ZAKE KAMA SIO KUTUKUZA U FREEMASONI BASI KUPOSHA WATU.
ANGALIA MASHAIRI YA ALIKIBA, HARMONIZE, NANDY, KISHA FANANISHA NA HUYO.
HIVI KUAJIRI MASHOGA KWENYE MEDIA, SI NDIO NJIA YA KU UPROMOTE?

AGENDA ZA WAJENZI HURU NI PAMOJA NA KUPUNGUZA IDADI YA WATU KWA KUTUMIA:
NDOA ZA JINSIA MOJA (HAKUNA UZAO)
VYAKULA VYA MAABARA(MBEGU ZA KISASA)
MLIPUKO WA MAGONJWA (KAMA CORONA)
nk
 
Mbona mashairi yao yana fanana sana labda Kiba na Nandy ndio tofauti, Sasa kwenye hizo ajenda lini Diamond aliunga mkono kimoja wapi ya hizo ajenda?
 
Jamaa anavaa mataka taka pete na chenu za fuvu ,kama siyo kwanini awe interested kuzivaa.
 
Nadny yule aliyesema anataka tango au nandy yupi unamsemea
 
Wasanii ni waongo mno hawana maisha ya hvyo tunayoyaona,ila sjui wanawezaje kuyaigiza hayo magari nani anawapatia
 
Almasi labda awe Mlozi tu, swala la Ujenzi huru hajafikia hizo level. Kuwa mjenzi huru si kama kunya.
 
Ukiwa ujenzi huru mafanikio yako yanakuwa gerentee tu ukiwa unafuata masharti then ukianza kupanda sana juu ndio masharti yanazidi kuwa magumu na yote unatakiwa uya tekeleze kinyume na hapo utaanza kushuka taratibu mpaka unaanza uteja then wao wanachukua chao as per aggreement unatangulia kwenye death chamber kusubiri hatma yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…