Hakuna mtihani mwepesi

Hakuna mtihani mwepesi

akashube

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2009
Posts
401
Reaction score
23
Hii ya kitambo lakini wacha tushtue mbavu kidogo:

Jamaa watatu walikuwa wakisafiri kupitia kwenye msitu mnene na kwa bahati mbaya wakakutana na majitu yanayokula watu na yakawakamata. Yale majitu yakawaambia 'sisi tuna mtihani ambao ukifaulu tunakuacha uende zako, la ukishindwa unaliwa.'

Basi yale majitu yakawatuma msituni wakiwa chini ya ulinzi kukusanya kila mmoja wao matunda kumi ya mti watakaochagua.

Baada ya muda mfupi mmoja wao akawa amefanikiwa kurudi na matunda aina ya Apple. Akaambiwa mtihani mlionao ni kuhakikisha kuwa unakula matunda yote kumi kwa kumeza bila kutafuna, moja moja lakini usionyeshe hisia yeyote katika uso wako.

Yule aliyekuja na apple akaogopa mno lakini akajizuia kuonyesha hofu yake, wakati huo huo yule wa pili akawa anakuja na matunda yake mkononi aina ya rasberry ambayo ni madogo na hayana kokwa. Yule wa kwanza alipoweka apple mdomoni kwake lilimzidi kinywa na hivyo akagugumia maumivu kwa hiyo akaliwa mara moja.

Huyu wa pili kuona hivyo akazuia hisia zake za hofu kubwa na akapewa mtihani ule ule wa kula matunda hayo moja baada ya jingine. Kutokana na udogo wa matunda hayo na kuwa hayana kokwa ndani alikula bila matatizo mpaka tunda la tisa.

Alipofika tunda la tisa akaangua kicheko kikubwa mno kwa ghafla hivyo na yeye akaliwa mara moja.

Mara wakajikuta wako ahera yule wa kwanza na wa pili. Yule wa wa kwanza akashangaa sana na kumuuliza 'imekuwaje wewe umeshindwa kula vile vijitunda?' Huyu wa pili akajibu na kusema ' nilimwona jamaa yetu wa tatu akija na mananasi'
 
Haki ya Mungu unanidai...yaaani wewe kiboko du nimecheka...sorry for spelling erroorrrrrrrrrr coz naandika huku nacheka...hii kali sana!
 
:biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1:yeah this is a good one.
 
Haki ya Mungu unanidai...yaaani wewe kiboko du nimecheka...sorry for spelling erroorrrrrrrrrr coz naandika huku nacheka...hii kali sana!

Ila usinidai pesa ya matibabu ya mbavu. weka barafu.
 
duh hii kali......umenifurahisha sana
 
Ama kweli ugumu wa mtihani ukipata matokeo

Haswaaa na sio muonekano wake.....wazoefu wa mitihani wameliona hilo...kumbe unaweza kuonekana mrahisi halafu kumbe mtihani huo huo mrahisi ukakugeuza dinner.
 
Duh hii kali, sasa mwingine angekuja na miwa(sugarcane) sijui ingekuwaje.
 
Hahahahaaaah hii kwa kweli imetulia.......mbavu zangu!!!
 
Jamani kweli kuna watu wanajua vichekesho na hii ni kali
 
hahhaha......asante maana umenifurahisha kweli!!!
 
Hii ya kitambo lakini wacha tushtue mbavu kidogo:

Jamaa watatu walikuwa wakisafiri kupitia kwenye msitu mnene na kwa bahati mbaya wakakutana na majitu yanayokula watu na yakawakamata. Yale majitu yakawaambia 'sisi tuna mtihani ambao ukifaulu tunakuacha uende zako, la ukishindwa unaliwa.'

Basi yale majitu yakawatuma msituni wakiwa chini ya ulinzi kukusanya kila mmoja wao matunda kumi ya mti watakaochagua.

Baada ya muda mfupi mmoja wao akawa amefanikiwa kurudi na matunda aina ya Apple. Akaambiwa mtihani mlionao ni kuhakikisha kuwa unakula matunda yote kumi kwa kumeza bila kutafuna, moja moja lakini usionyeshe hisia yeyote katika uso wako.

Yule aliyekuja na apple akaogopa mno lakini akajizuia kuonyesha hofu yake, wakati huo huo yule wa pili akawa anakuja na matunda yake mkononi aina ya rasberry ambayo ni madogo na hayana kokwa. Yule wa kwanza alipoweka apple mdomoni kwake lilimzidi kinywa na hivyo akagugumia maumivu kwa hiyo akaliwa mara moja.

Huyu wa pili kuona hivyo akazuia hisia zake za hofu kubwa na akapewa mtihani ule ule wa kula matunda hayo moja baada ya jingine. Kutokana na udogo wa matunda hayo na kuwa hayana kokwa ndani alikula bila matatizo mpaka tunda la tisa.

Alipofika tunda la tisa akaangua kicheko kikubwa mno kwa ghafla hivyo na yeye akaliwa mara moja.

Mara wakajikuta wako ahera yule wa kwanza na wa pili. Yule wa wa kwanza akashangaa sana na kumuuliza 'imekuwaje wewe umeshindwa kula vile vijitunda?' Huyu wa pili akajibu na kusema ' nilimwona jamaa yetu wa tatu akija na mananasi'

hawajui hao wa kuzimu! Mwenzao aliambiwa atengeneze juisi ya nanasi halafu anywe! Wajinga ndo walikwenda kuzimu...
Walisahau kuwa '' ukubwa wa pua si wingi wa kamasi''
 
Halafu ikikupalia tu umeliwa.
 
hawajui hao wa kuzimu! Mwenzao aliambiwa atengeneze juisi ya nanasi halafu anywe! Wajinga ndo walikwenda kuzimu...
Walisahau kuwa '' ukubwa wa pua si wingi wa kamasi''

kweli aisee maana jamaa hakuonekana kuzimu. alishinda mtihani
 
Back
Top Bottom