CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,872
- 9,263
Huu ndo ukweli ambao hutakaa uambiwe ila ni ukweli mtupu na iko hivyo.
Hakuna mtu atakae kuambia fanya hiki au fanya kile UTAJIRIKE au KINALIPA kama yeye hatapata chochote kile kutoka kwako.
Mimi nikija kukuhamasisha kufuga kuku jua nitauza vifaranga hilo ndo lengo kuu hiyo tajirika ni entry point tu.
Nikikuambia panda miti ya mbao utajirike baso jua nitakuuzia miche ya hiyo miti na mimi nitafaidika hapo.
Katika mazingira ya Kawaida sio rahisi mtu akuambie fanya kile utajirike kama yeye hatanufaika.
Ukiona anakuambia fanya kile utatoka na yeye hakifanyagi basi jua ana wrong information au alisha jaribu akapata hasara sasa anatafuta wafuasi au anataka kukutanguliza ili ajifunzie kwako.
Mengi hata siku moja kwenye mikutano yake ya kuhamasisha vijana wajiajiri huwezi sikia anakuambia anzisha kiwanda cha maji, anzisha kituo cha Radio au anzisha Gazeti.
AZAM hata siku moja hawezi kukuambia fungua kiwanda cha Juice au pika mandazi au mikate au anzisha biashara ya kupack maji.
Wengi huwa wanavutiwa na maneno mawili tu TAJIRIKA na INALIPA.
Watu wa Network Marketing huwa ni mabingwa wa kutumia TAJIRIKA ila sasa anaye kuamboa tajirika unakuta shati limepauka vibaya mno ila anakuhubilia tajirika. Ukiona hivyo jua yeye kuna namna atafaidika na wewe kuingia.