Ntaganda boy
Member
- Jan 16, 2016
- 90
- 59
Na zaidi pia Haipo Dhana ya Kujiua kwa Makusudi, kila siku ni taharuki na hamaki katika mazingira yanayotuzunguka. Watu wengi wana nadhalia zao na nadhalia hizo huchochea jamii kuishi na taharuki wanayoipata baada ya mtu kujiua au kuua na katika kujiua kuna njia mbalimbali mfano; kujirusha ghorofani, Majini, siraha, sumu, kamba n.k.
Moja ya kichwa cha habari kilichotikisa kichwa changu kilikua kimenukuliwa baada ya mtu kujiua kwa kujirusha ghorofani na kusema kuwa '' Amejirusha Makusudi Ghorofani-Polisi''Nianze na kusema kuwa hakuna kujiua kwa makusudi (Taarifa ya polisi ilivyosema), changamoto au magonjwa ya akili ndio msukumo mkubwa na namba moja ya watu kujiondoa uhai duniani. Na hii dhana ya magonjwa ya afya ya akili au saikolojia ndio huashiria kuwa hakuna muoga wa kufa maana matokea ya kujiondoa uhai huambatana na kukosa thamani ya kuishi.
Dhana ya kujiua makusudi inakuja kwa sababu dalili za afya ya akili sio rahisi kuziona kwa macho hasa mtu anapokua katika hatua za awali zaidi itajulikana kuwa mtu ana tatizo kama kuna mabadiliko ya kitabia, kihisia, kifikra na kiimani. Hii ina maelezo mengi zaidi.
Kwanini Taharuki
Aliyejiondoa uhai alikua mtoa ushauri nasaha na hii ndio imeshtua umma zaidi maana mtoa huduma kwa wengine ndio amejiondoa uhai. Hili nilitolee maelezo kitaalamu zaidi.
Katika taaluma ya afya ya akili inayowahusisha watu kama Wanasaikolojia, Wanasihi (Counsellors), Psychiatrists, na wengine watoa huduma jamii saidizi za saikolojia kama Ustawi wa Jamii, Madaktari, Walimu n.k. Kuna sheria juu ya watoa huduma zinazowataka wao pia kuwa wanapata huduma za unasihi/saikolojia yaani mtoa huduma anapaswa kupata huduma pia (Every Therapist has personal Therapist or Consultant) na ni sheria za kimataifa za wanasihi ndio maana Mnasihi au Mwanasaikolojia anakua chini ya Mwanasaikolojia mwingine.
Sheria hii haitekelezwi na watoa huduma wengi wa afya ya akili na kuna uwezekano pia wakawa hawajui juu ya sheria hii na iliwekwa ili kumsaidia mtoa huduma na yeye kutua mizigo ya watu lakini pia kushughulikia changamoto zake binafsi (Unfinished businesses).
Nani Msimamizi wa Watoa Huduma
Pamoja na kuwepo na wapata huduma, wahitaji huduma na watoa huduma wengi ila bado Tanzania haina bodi ya serikali inayoratibu wanasaikolojia na wanasihi ambayo ndio inapaswa kuwa msimamizi mkuu wa sheria na taratibu zote katika usajili wa wataaluma na watoa huduma. Kuwepo kwa bodi inayoratibu inaweza kusaidia kupunguza vifo vya wataaluma na kuwepo kwa huduma sahihi na bora maana sasa hivi watu wengi wamejivika koti la uanasaikolojia, ushauri nasihi na nasaha ingali sio wataalamu na hawajui ufanyaji kazi wa nasihi na saikolojia halisi.
Nielezee tukio la kujirusha ghorofani, kuna aina nyingi za magonjwa na changamoto za kisaikolojia zinazomfanya mtu kuwa na msukumo na mawazo ya kujiondoa uhai, baadhi ya changamoto hizo ni Sonona (Depression), Hisia mseto (Bipolar), Sikizofrenia (Schizophrenia), Mgandamizo wa mawazo (Distress) Hasira mlipuko (Anger) Wasiwasi (Anxiety) n.k. Magonjwa haya ndio yanatoa tamko juu Hakuna Muoga wa Kufa Diniani. Hii inamaanisha kuwa mtu anapaswa atafute huduma pale tu anapokua na tatizo lolote, wenzetu wa nchi zilizoendelea watu wana wanasaikolojia wao (Personal Therapist) kama ilivyo mtu kuwa na mwanasheria wake, ni swala la kujenga utamaduni tu.
Je Aliyejiua Baada ya Kuchepuka, Nayo Iko Kundi Gani
Ukisoma aya ya juu, utaelewa ni jinsi gani jamii inauhitaji mkubwa wa huduma hasa elimu ya kuwafunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto za kisaikolojia. Mfano; kwa aina ya kifo cha kunywa sumu baada ya kuchepuka kwa kusikia tu hata kama wewe si mtaaluma wa saikolojia utaelewa kabisa hapo inawezekana marehemu alikua na changamoto ya Ugonjwa wa Wasiwasi au Hasira pamoja na mambo mengine yanayoshahabiana na hayo.
Nani wa Kuwajibika Juu ya Hili
Hadi sasa kila mtu anatakiwa kuwajibika katika kuilinda afya yake ya akili, jamii ipeane elimu kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa kupitia watu wenye taarifa sahihi za afya ya akili.
Wizara ya Afya na TAMISEMI, ni wakati sasa wa kupeleka watoa huduma za afya ya akili katika ngazi za msingi za utoaji wa huduma za afya ili wananchi waweze kupata huduma na taarifa stahiki. Uajili wa wanasaikolojia na wanasihi ni sehemu ambayo nchi imechelewa ila bado haijachelewa sana hivyo bado nafasi ipo ya kutoa ujira kwa wataaluma wa afya ya akili ili waihudumie jamii.
Wizara ya Elimu, hapa tunasnza na uwepo wa taarifa juu ya afya ya akili katika shule za ngazi zote yaani msingi, sekondari hadi vyuo vya kati na vyuo vikuu. Uwepo wa Wanasihi wa kuwanasihi wanafunzi katika taaluma zao lakini pia wanapopitia changamoto zozote za maisha na masomo. Vyuo vya kati na vikuu, viwe na sheria za kulazimisha waangalizi wa wanafunzi wawe na mafumzo ya kutoa huduma za kisaikolojia na unasihi.
Tukumbuke watu wengi wanajiondoa uhai sababu ya afya ya akili ila matukio tunayoyasikia ni machache sana.
Asante kwa kusoma, mtumie pia mwenzio naye apate elimu hii.
Bosco Bosco
Mwanasaikolojia Mnasihi (Counselling Psychologist)
+255759238035

Upvote
1